2015-09-10 16:15:00

Kituo kikubwa zaidi cha nishati ya jua barani Afrika kimezinduliwa nchini Ghana


Kituo kikubwa zaidi cha nishati ya jua barani Afrika kimezinduliwa nchini Ghana. Kituo hicho kilichopewa jina la Nzema, kimezinduliwa magharibi mwa nchi hiyo. Kwa mujibu wa serikali ya Ghana kituo hicho cha nishati ya jua, kimejengwa kwa kiasi cha karibu Euro milioni 300, na kinazalisha umeme wa megawati 155, na Kituo cha nishati ya jua kinahesabiwa kuwa moja ya vituo vikubwa vya nishati duniani, kutokana kwamba hadi sasa ni vituo vitatu vikubwa kama hivyo vilivyopo duniani, vyote viko barani Afrika.

Kuanzishwa kituo cha nishati cha Nzema nchini Ghana, kunatajwa kama mafanikio muhimu katika uga wa nishati mpya barani Afrika, ambapo sasa nchi nyingine za bara hilo zinaweza kutumia njia hiyo kumaliza tatizo la umeme ambalo limekuwa sugu kwa mataifa hayo. Kabla ya hapo Ghana ilikuwa ikijidhaminia nishati ya umeme kupitia vyanzo vya maji, hata hivyo kutokana na kwamba taifa hilo limekuwa likikabiliwa na ukame wa mara kwa mara, vyanzo vya maji havikuwa tegemeo katika kukabiliana na tatizo hilo.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.