2015-09-07 14:59:00

Rwanda: Tuzo Ikwita - Izina kwasababu ya kulinda na kutunza hifadhi za utalii


Jumamosi 5 Septemba 2015 Nchini Rwanda kumefanyika sherehe juu ya Utalii ambapo katika sherehe hizo walipata  kumuona mtoto wa Sokwe, akirudishwa kwa mama yake katika mlima wa Bisoke Kaskazini kwenye Mbuga ya wanyama Sherehe hizo zimefanyika katika Eneo la Ikwita  -Izina.   

Kwa miaka  11  eneo la Ikwita – Izina limekuwa eneo kubwa la utalii nchini Rwanda, unao vutia na kusifiwa  na dunia kwa hatua kubwa wanayoifanya ya kuifadhi masokwe ambao kwa miaka michache iliyopita wamekabiliwa na changamoto la kutokomea.

Kwa mujibu wa mkuu wa idara ya utalii katika Bodi ya  Maendeleo Rwanda, Bwana Faustin Karasira, Alisema kwa mara ya kwanza mwaka huu, wananchi, watapewa tuzo kwa juhudi zao katika hifadhi na kudumisha, kulinda na uendelezaji wa sekta ya utalii, na pia Rwanda imewakaribisha  zaidi wa viongozi wakuu wanchi 32 kutoka kote duniani, na wakazi tokea pande zote za nchi  walifika kusheherekea tukio hilo la mtoto gorila akirudishwa kwa mama yake katika msitu ambamo wanaishi masokwe hayo.








All the contents on this site are copyrighted ©.