Jumanne ambayo ni tarehe Mosi Septemba, Papa Francisko, atazindua kwa mara ya kwanza Siku ya Dunia ya Sala ya Kuombea Huduma kwa viumbe, kama alivyotangaza katika barua yake iliyochapishwa tarehe 6 Agosti.
Katika barua hiyo , Papa Francisco alilihimiza Kanisa Katoliki kuungana na Mkuu
wa Kanisa la Kiekumeni la Kiotodosi, Patriaki Bartholomayo I, ambaye kwa namna ya
kipekee ameonyesha kujali mustakabali wa viumbe hai. Na kwa maoni yaliyotolewa na
mwakilishi wake wa Papa , Askofu Mkuu Ioannis wa Pergamo, kama mchango wake wakati
wa kuandikwa Waraka" Sifa kwako kwa ajili ya utunzaji wa dunia makazi ya wote ” Laudato
Si, Papa alitangaza maamuzi yake ya kuanzisha katika Kanisa Katoliki, Siku ya Maombi
kwa ajili ya kujali huduma kwa viumbe Dunia, tarehe mosi Septemba. Tarehe ambamo
Kanisa la Kiotodosi imekuwa ni desturi ya kuombea viumbe kwa miaka kadhaa sasa.
Waraka wa Papa , ulitaja madhumuni ya Siku ya Dunia ya kuombea kujali huduma kwa viumbe,
kwamba ni kutoa muda kwa waamini, kwa mtu binafsi na jamii kwa ujumla, nafasi ya
kufaa kuthibitisha wito binafsi wa kuwa mawakili wa viumbe na kumshukuru Mungu kwa
kazi ya ajabu ya mikono yake, ambayo aliikabidhi chini ya huduma ya binadamu. Hivyo
siku hii ya sala ya kuombea kujali huduma kwa viumbe, pia inatuhimiza kutafuta msaada
wa Mungu kwa ajili ya ulinzi wa viumbe, na vile vile kuomba msamaha wake kwa dhambi
tulizofanya dhidi dunia ambayo ni makazi ya viumbe wote. . Aidha Papa anafurahi kwamba,
maadhimisho ya siku hii, yanakwenda sambasamba na desturi ya Kanisa la Kiorthodox
na hivyo inakuwa ni fursa ya thamani kubwa, kama tukio jingine linaloshuhudia mpanuko
wa umoja wa Wakatoliki na Waotodosi kama ndugu moja.
Barua ya Papa Francisco alieleza na kuonya kwamba, tunakiishi kipindi hiki ambamo Wakristo wanapambanishwa na changamoto nyingi katika kufanya maamuzi thabiti. Na hivyo inakuwa ni lazima kwa kila Mkristo, kufanya kila jitihada, katika utoaji wa jibu la pamoja, nzito thabiti la kuaminika na ufanisii zaidi.
Papa alionyesha tumaini lake kwamba, katika siku hii, pia Makanisa mengine na Jumuiya za kikanisa, zitashiriki katika Ibada hii, kama ilivyoshauriwa na Baraza la Makanisa Duniani.
Barua ya Papa inawatia shime watu wote ikisema kwamba, , kama mtu binafsi, au
kama taasisi, au kama jamii ya watu, tunahitaji mabadiliko ya moyo kwa ajili ya kuhifadhi
na kulinda sayari ya dunia kwa watoto wetu na vizazi ambavyo bado kuzaliwa. Mabadiliko
ya Tabianchi ni mjadala unaohitaji unyenyekevu na utii kwa manufaa ya wote, kama lilivyo
sema pia Baraza la Maaskofu Katoliki la Marekani mwaka 2001.
Kwa hiyo, Barua ya Papa inahimiza Tume za Liturujia za kanisa Katoliki, kukiingiza
kipengere hiki katika maombi ya ibada kwa ajili ya kutoa msisitizo katika wajibu
binadamu kulinda viumbe wote wa Mungu na kwa Maadhimisho ya Sikukuu kwa Mtakatifu
Francis na Mtakatifu Isidore.
Kwa ajili ya uzinduzi wa Liturujia ya Siku ya Kuombea huduma ya Viumbe, utakaofanywa na Papa Francisko na hapa Vatican, mwaliko umetolewa kwa maaskofu, mapadre, watawa na walei kufika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro majira ya saa kumi na moja za jioni, kushiriki katika Liturujia ya Neno, maalum kwa ajili ya Kuzindua Siku ya Dunia ya Kuombea huduma kwa ajili ya viumbe hai vya Mungu.
All the contents on this site are copyrighted ©. |