2015-08-31 16:25:00

Kifo cha Askofu Pierfranco Pastore ,maisha yake katika vyombo vya mawasiliano


Taarifa kutoka Vatican zinasema Jumapili 28 Agosti Monsinyo Pierfracon Pastore aliyekuwa na umri wa miaka 88 amefariki dunia.

 Askofu  Pastore  aliwahi kuwa Katibu wa Baraza la kipapa katika Mawasiliano, na kufanya kazi radio Vatican kwa miaka mingi.

Tangu 2003 alikwenda pensheni  lakini aliendelea kuwa mshauri mwema kwa waandishi wa habari na wahudumu wa vyombo vya mawasiliano kila mara walipokuwa wanahitaji msaada wake.

Ibada ya mazishi itafanyika Roma Jumanne 1 Septemba kwenye Kanisa  liloko katika kituo cha Umoja wa vijana Katoliki kabla ya kusafirishwa mwili kwenda Novara Italia.








All the contents on this site are copyrighted ©.