2015-08-28 15:54:00

Watumishi 1,200 wa Afya kupata ajira kutoka Taasisi ya Benjamin Mkapa


Hivi karibuni Julai 27 hadi Agosti 25 Mwaka huu Taasisi ya Benjamini Mkapa HIV/AIDS (BMAF),iliandaa mafunzo ya mwezi mmoja katika Mkoa wa Shinyanga kwaajili watumushi wa Afya . Taarifa kutoka Gazeti la NIPASHE, zinasema wakati wa  kufunga mafunzo ya watumishi wa afya 22 wa kada mbalimbali za matibabu ya uuguzi na ufamasia, Mratibu wa Mafunzo wa taasisi hiyo, Dk. Shabani Kingazi, alisema Taasisi ya Benjamin Mkapa imeajiri watumishi wa afya 1,199 ambao wanafanya kazi katika wilaya 142, vituo 43 vya kufundishia na hospitali za mikoa 23 kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa watumishi wa afya katika maeneo ya vijijini nchini.

Mafunzo hayo ya mwezi mmoja  kwa mwaka huu kwa watumishi hao ambao watapelekwa katika kufanya kazi mkoani Simiyu,  yalijumuisha mafunzo ya darasani na ya vitendo, na ni matumaini ya  kuwa watakwenda kuwa mfano mzuri huko waendako kwa kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wagonjwa waishio na Virusi vya Ukimwi na Ukimwi, alisema.

 Naye mgeni rasmi kwenye tukio hilo , Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Nuru Mpuya, aliwaasa wataalam hao kufanya kazi kwa bidii na maarifa zaidi kwa faida ya watakaowahudumia na taifa kwa ujumla. 

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.