Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki (KCCB), Askofu Philip Anyolo, ametangaza
rasmi juu ya ujio wa Papa nchini Kenya kwamba itakuwa mwezi Novemba 2015. Hilo limo
katika barua yake kwa Waamini Wakristo aliyoitoa kwa niaba ya Maaskofu, Alhamis ya
wiki hii tarehe 27, Agosti, 2015. Askofu Anyolo kasema, "Baba Mtakatifu amekubali
mwaliko wa Maaskofu wa kuitembelea Kenya mwezi Novemba 2015.
Anyolo Askofu, wa JImbola Homabay, pia anasema , ziara ya Papa ni ziara ya kichungaji,
nahivyo Kanisa litashirikiana na Serikali ya Kenya, katika maandalizi na ufanikishaji.Askofu
Anyolo ameeleza na kuomba sala za waamini na msaada wa kihali kwa ajili ya kufanikisha
ziara ya Papa nchini Kenya.
Maaskofu wa Kenya katika ziara yao y akitume ya kila baada ya miaka mitano katika
Ofisi za Idara ya Curia ya Roma na Kiti Kitakatifu , waliyoifanya hapo 13-17th, Aprili,
2015, walitoa mwaliko kwa Baba Mtakatifu alitembelee taifa la Kenya.
Katika ziara hii ya kwanza kwa Papa Francisco kuzuru bara la Afrika, pia atatembelea Uganda na a na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
All the contents on this site are copyrighted ©. |