2015-08-27 07:43:00

Expo Milan 2015- Papa atoa msaada kwa wakimbizi Jordan


Baba Mtakatifu Francisco kwa upendo na  huruma ya Kibaba , ametoa msaada wa Euro 68,000 kwa wakimbizi wa Syria na Iraki wanaoishi katika mpaka wa Yordani.  Fedha hizo ni sehemu ya fedha iliyokusanyika katika banda la Vatican katika  Maonyesho ya Kimataifa ya Expo Milan 2015, ambako Vatican ilipewa nafasi ya kuweka banda lake tangu mwanzo wa  maonyesho haya yaliyoanza mwezi June. Mamia ya maelfu ya watu wametembelea banda  la Vatican  na bado wanaendelea kumiminika katika banda hilo kila siku.

Fadhila za Papa kwa wakimbizi wa Yordani zitawafikia walengwa kupitia mkono wake wa Baraza la Kipapa la Misaada “Cor Unum”, kukidhi walau kwa kiasi fulani,  mahitaji ya familia za wakimbizi na hasa wazazi walioandamana na watoto wao wadogo kutoka Syria na Iraki, ambao kwa sasa wanaishi mpakani mwa Yordani, katika  mazingira magumu, kama waathirika wa mgogoro wa vita, Mashariki ya Kati.

Sehemu kubwa ya fedha iliyopatikana inatokana na mauzo ya vitabu mbalimbali  vya Vatican, ikiwemo kitabu kipya, chenye kuwa na waraka mpya wa Papa Francisco” Ensiklika” juu ya utuzaji wa mazingira “Laudato Si "ambacho  nakala zake zimeuzwa zaidi ya 5,000 katika lugha ya Italia. Kwa lugha kihispania 140, kiingereza nakala 340 kwa na Kifaransa nakala 380.








All the contents on this site are copyrighted ©.