2015-08-26 14:28:00

Shirika la misaada ya watoto la toa masikitiko juu ya afya ya watoto wakimbizi


 Kijana wa miaka 15 kufariki dunia wakati wa kuvuka Bahari  kuja Ulaya, umeonyesha dalili wazi juu ya maelefu ya watoto wakimbizi huko Libya wanavyoteseka , kwa kupigwa,  kufanyishwa kazi yenye nguvu bila ya chakula hata kukosa  maji ya kunywa.   

 Hayo yalielezwa na Mkurugenzi wa mpango wa saidia watoto (Save Children) wa nchini  Italia Bi Raffaella Milano ya  kwamba  tangu mwanzo wa mwaka wamewapokea watoto 7,600 bila kusindikizwa na mtu yeyote,  wengi wao ni  vijana wadogo kutoka nchi za Eritrea, Somalia na nchi nyinginezo .

Wanafika wakiwa na vidonda na makovu mengi yaliyotokana na  vipigo na  ukatili mkubwa kwenye miili yao .Aliendelea wengi wao wanaliofika katika vituo vya huduma ya kwanza kabla ya kusafirishwa kwenda vituo vingine kwenye ufukwe wa visiwa vya Italia, ni vijana waliodhoofika sana hawana nguvu , kutokana na utapia mlo na makovu mengi katika miili yao.

Maelezo ya Watoto hao ni kuanzia miaka 11 na kuendelea, wanasafiri safari ndefu kutoka makwao, hadi kukatisha nchi ya Libia wapate kuja Ulaya, na wanawalipa  watu ela nyingi wanaofanya biashara haramu ya binadamu.

Bi Raffaella Anasema ni muhimu hawa watoto wakapokelewa na kulindwa  na kupata matibabu muhimu ya afya ili waweze kupona majeraha  ya kisaikolojia  na ya kimwili. Lakini zaidi ya hayo anatoa wito ya kwamba  ni muhimu Jumuiya za umoja wa Ulaya kufanya kila liwezekanalo kutafuta mbinu za haraka za  kuweza kuzuia na  kuokoa watoto wengi ambao wako katika misafara ya kutoka makwao  kuelekea Libya kabla hawajajikuta katika mikono ya wafanya biashara  haramu ya binadamu.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.