Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki Uganda (UEC) ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Gulu, Askofu Mkuu John Baptist Odama, amemwelezea Marehemu Askofu Paul Kalanda, Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki la Fort Portal, kwamba alikuwa ni mtu muhimu, mshauri mkubwa, mmisionari na nembo ya hekima. Maelezo ya Askofu Mkuu Odama yalifuatia taarifa za kifo cha Askofu Kalanda, aliyefariki katika usingizi, asubuhi ya Jumanne iliyopita Agosti 18, katika makazi yake ya Villa Maria, Jimbo la Masaka, Uganda.
Askofu Mkuu Odama akirejea taarifa za kifo cha Askofu Kalanda, amesema, alizipokea kwa huzuni kubwa, kwa kuondoka kwa Mtendaji mkuu huyu wa Kanisa aliyempenda Kristo na kanisa lake bila kujibakiza. Na kwamba, wakati Askofu Kalanda akiwa Mwenyekiti wa UEC, alitumikia kwa upendo sio tu kwa Kanisa lakini kwa taifa zima la Uganda. Ni mtu aliyependa umoja, amani na maendeleo kwa taifa lake la Uganda. Na hivyo Kanisa limepoteza mmoja wa watu wake mashuhuri, jasiri na muhimu. Mchango wake ulikuwa bado unahitajika hasa kwa wakati huu wa mchakato wa mabadiliko nchi Uganda.
Askofu Paulo Kaloanda alizaliwa Februari 24, 1927 katika kijiji cha Buwunde, Jimboni Masaka , kwa familia Baba Simon Zilyawukanya Kalanda na Mama Agnes Nakachwa , akiwa mmoja wa watoto watano, wavulana wanne na binti mmoja.
Baada ya kuhitimu masomo kwa ajili ya Upadre, alipadrishwa Desemba 21, 1957 na baada ya hapo aliendelea na masomo yake katika Chuo Kikuu Kipapa cha Gregorian cha mjini Roma ambako alipata Shahada ya Uzamivu katika falsafa (PhD) ya sheria za Kanisa mwaka 1961.Na baada ya hapo kurudi nchini mwake kulitumikia Kanisa.
All the contents on this site are copyrighted ©. |