2015-08-20 14:18:00

Siasa na isiwe utendaji wa kisirisiri na ujanja bali haki na ukweli


Katibu Mkuu wa Sekretariati ya Baraza la Maaskofu Katoliki Italy , Askofu Nunzio Galantino , hivi karibuni akizungumzia mwelekeo wa siasa nchini Italy alionya kwamba, ni kweli kwamba taifa bila siasa ni taifa lililokufa. Na  utendaji wa kisiasa, si utendaji wa kisirisiri au hila lakini inapaswa kuwa ukweli haki. Hivyo utendaji wa kisiasa ni utendaji usiokwepeka katika jamii, kwa kuwa ni mfumo wa maisha katika msingi wa kutetea na kulinda ubinadamu. 

Askofu Galantino alieleza na kukumbusha kwamba, mpaka sasa hakuna mtu aliyekwisha vumbua mbadala,  kwa ajili ya utendaji wa  taasisi za kisiasa, sheria, demokrasia. Hivyo Jamii ni lazima iwe na mfumo wa utawala wa kisiasa, kwa ajili ya kuwaunganisha watu , yakiwemo makundi ya kidini kama Wakristo. Na watu wote ni lazima kujua nini maana ya utawala wa kiserikali na  juu ya yote, utendaji wa haki na sheria. 

Maoni ya Mons. Galantino, yalitolewa na Rais wa Chama cha  Trentino Alcide De Gasperi, Joseph Tognon, katika Mkutano wa chama hicho , kama tahadhari ya kuepuka vurugu na mtafaruko kati ya wananchi na serikali ,kutoka una utata uliopo sasa hasa wimbi la wahamiaji wanao ingia Kusini mwa Italia.  

Monsinyori Galantino , ametazama kwa kina maendeleo ya kisiasa tangu nyakati za nyuma za vita vya dunia hadi nyakati hizi, ambamo amegundua kwamba,  Kanisa katika kipindi cha baada ya vita, liliona uzuri wa ukarimu miongoni mwa watu, na hivyo kuijenga tabia ya watu wa Italy, kitaifa katika moyo wa ukarimu hasa wakati wa matukio muhimu ya kisiasa. Katika kipindi hicho cha baada ya vita kuu ya dunia, kulijengeka  mfumo wa ushiriki wa umma wa hali ya  juu, ikiwa pamoja na maandamano yaliyothibitisha ukweli wa ujumbe katika hatua inayotakiwa kuchukuliwa kama huduma na umma.  

Askofu Galantino aliendelea kutazama mwelekeo uliojenga  heshima na sifa ya  kanisa kuwa karimu, baada ya vita hivyo vya dunia, na kutoa wito kwa  kizazi kipya cha manaibu na maseneta" na vyama vya wafanyakazi , na mashirikisho yanayounganisha vyama vya kisiasa, na  vyama vya kijamii na  mashirika ya dini, wote kutenda kwa  ukarimu na haki kama ilivyokuwa katika kipindi cha miaka ya baada ya vita kuu ya dunia.

Aidha amewaasa Wakatoliki, kuingia katika utendaji wa kisiasa na siyo kuwa watazamaji au watu wa  kati, wasiokuwa na upande wowote,  watu nusunusu katika utoaji wa maoni kwa kufikiri kwamba huko ndiko kuwa Mkatoliki mzuri. Amekemea Mkatoliki kuwa mtu asiyekuwa na msimamo thabiti, si upande wa utawala au  upande wa upinzani, au katika kueleza ukweli. Amesema Mkatoliki anayejiweka kando ya utendaji wa  kisiasa au kisanyansi au teknolojia mpya, mwenye woga wa kufurahia au kukemea utendaji unaofanyika, kuwa mtu mwonga, kuchochea utangazaji wa Injili ya Bwana kwa uhodari zaidi katika mifumo ya maendeleo ya kiuchumi na kiteknolojia, huyo si Mkatoliki safi

 Anasema , Mkristo bora ni yule anayejiingiza katika utendaji wa kila jambo, kuona uhalali wake au kasoro zake na kutoa maoni yake, kukosoa au kukubali , ili katika hayo aweze kuwapa watu wengine pia habari njema ya wokovu wa Kristo, ambao ni upendo na utendaji wa haki katika utumishi wa umma, katika mipango na sera zote za kijamii, kisiasa , kiuchumi na kidini pia. Kwa namna hiyo inakuwa ni kuuweka utumishi na huduma binafsi kwa ajili ya manufaa ya wengine.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.