Mtazamo wa 2050 kwa misitu na hali zake – Ni mada itakayozindua Tathmini ya Dunia juu ya Rasilimali za Misitu 2015
Haja ya serikali, asasi za kiraia na sekta binafsi kuongeza uwekezaji katika misitu,
itakuwa ni kipengere muhimu kwa maendeleo endelevu katika Kongamano la Dunia la XIV
la Misitu litakalo fanyika Durban, Afrika Kusini, kuanzia Septemba 07-11 mwaka 2015.
Kongamano linaongozwa na Madambiu ; Misitu na Watu: Uwekezaji katika mstakabali wa
Maendeleo endelevu ,ambamo washiriki watajadili njia za kuongeza uwezo kamili wa
misitu na kuinua ustawi wa wakazi vijijini, kujinasua na umaskini, kama kitendo pia
cha kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na uhamasishaji wa teknolojia mpya
na bidhaa mbadala.
Mawaziri na wakuu wa vyombo vya kitaifa na kimataifa watakuwa kati ya washiriki wa
Kongamano hili litakalo jumuisha pamoja maelfu kadhaa ya watu katika kongamano hili
lenye kufanyika kila baada ya miaka sita. Kongamano la mwaka huu linafanyika mjini
Durban Afrika Kusini, kwa msaada wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa
(FAO), ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika Afrika, tangu kuanzishwa kwake mwaka 1926.
FAO, inataarifu kwamba, kati ya mambo muhimu yatakayo fanyika ni pamoja na uzinduzi
wa Tathmini ya Dunia ya Rasilimali ya Misitu 2015, ambayo itaonyesha jinsi misitu
ya dunia nzima ilivyo badilika katika kipindi cha miaka 25 iliyopita na kutoa taarifa
za karibuni juu ya hali ya usimamizi endelevu wa misitu.
Matokeo Kongamano hili la Matazamio ya 2050, yanatarajiwa kupendekeza uwezo wa kuimarisha
mchango wa misitu na uoto wake kwa mustakabali endelevu na kusaidia kusafisha barabara
kwa ajili ya protokali mpya juu ya mabadiliko ya tabianchi, inayotazamiwa kupitishwa
katika Mkutano wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa juu ya Mabadiliko ya Tabianchi,
katika Mkutano wa Kilele utakao fanyika mjini Paris Desemba, 2015.
All the contents on this site are copyrighted ©. |