Jumatano 19 Agosti Baba Mtakatifu Francis katika katekesi juu ya Familia, ameongelea kipengele cha "kazi" baada ya wiki iliyopita kuongelea juu ya "mapumziko" katika maisha ya familia. Alisema mapumziko na kazi vinafanya sehemu ya mpango wa Mungu.
Kwa walio wengi wanasema kazi ni muhimu katika kutunza familia na katika kuwakuza watoto. Ni mfanyakazi ambaye anaishi katika jamii bila kutegemea wengine, na pia kazi hata za nyumbani zinaleta manufaa kwa jamii nzima.
Lakini kazi hizo tunajifunzia wapi? Aliuliza Baba Mtakatifu na kutoa jibu kuwa awali ya yote kazi ni kujifunza kutoka ndani ya familia. Familia inafundisha kazi kwa mfano wazazi baba na mama wana fanya kazi kwaajili ya manufaa ya familia na jamii.
Baba Mtakatifu aliendelea kueleza katika injili ya familia Takatifu ya Nazaret inaonesha jinsi familia ya Yesu ilikuwa ya wafanyakazi, maana Yesu mwenyewe aliitwa mtoto wa seremala (Mt,13,55) na hata kuitwa yeye mselemala.
Na pia Mtaktifu Paulo katika barua yake aliwaonya wakristo ya kuwa “asiye fanya kazi na asile”(2,Ts 3,10). Maonyo hayo yalitokana na uzushi wa dini za uongo, waliokuwa wakitaka kuishi wakitegemea ndugu zao kaka na dada bila kufanya lolote (2Ts 3,11). Lakini shughuli za kazi na maisha ya kiroho vilikwenda kinyume na mawazo hayo .
Baba mtakatifu alisistiza ya kuwa inabidi kutambua vema hili, kazi na sala vinapaswa kwenda sambabamba , kama anavyofundisha Mtakatifu Benedikto.
Ukosefu wa kazi unaharibu hata roho kama vile ukosefu wa sala unavyoharibu utaratibu mzima wa maisha. Kufanya kazi kunaleta tija na heshima ya utu na kutambua kuwa umeumbwa kwa mfano wa Mungu, Na Wanasema kwamba kazi ni kitu kitakatifu.Utafutaji wa ajira ni jukumu kubwa la binadamu na jamii ambayo haiwezekani kuachwa katika mikono ya walio wachache na katika masoko ya wanao miliki.
Ukosefu wa nafasi za kazi maana yake ni kuleta hasara kubwa katika jamii. Alirudia baba mtakatifu kusema ,kazi na mapunziko ni vitu vilivyo katika mpango wa Mungu muumbaji. Katika Biblia, kitabu cha mwanzo wazo kuu la ardhi kama bustani ilikabidhiwa kuwa kazi ya binadamu (Mw 2,8.15).
Baba Mtakatifu aliendelea “siku ile Bwana Mungu alipoziumba mbingu na nchi hapakuwa na mche wa konde , wala mboga ya konde haijachipuka bado kwa maana Mungu alikuwa haijainyeshea nchi kavu , wala hapana mtu wa kuilima! (Mw 2,4b).
Baba Mtakatifu alionyesha kuwa hii siyo kitabu cha riwaya bali maono ya Mungu, na sisi tunalojukumu la kutambua hadi mwisho jambo hili.
Akirejeea katika Enskilika yake ya Laudato Si “sifa kwa Mungu”. Alisema inashauri juu utunzaji wa mazingira kwa ujumla ,na inatoa ujumbe huo wa uzuri wa nchi na heshima ya kazi , vitu ambavyo vimekuwepo kukamilishana.
Kazi ikijitenga na mpango wa Mungu na binadamu pia wakakosa muungano wa kiroho, maisha hayo uchafua kila kitu, hewa maji , mimea na chakula, na Maisha ya binadamu uharibika zaidi ya hayo matokeo yake wanaohangaika ni wale familia masikini.
Baba matakatifu alitaja kuwa, Mashirika ya kileo ya kazi, inaonyesha wakati mwingine kuwa familia ni mzigo katika uzalishaji, na tatizo hili linawakumba watoto na wazee.Wasiwasi wa Baba Matakatifu Francisa ni juu ya wanahusika katika utoaji ajira na kusema kuwa utaratibu wao ni kwaajili ya ubinafsi.
Aliendelea kuonyesha juu ya familia inavyokabiliwa na changamoto, na pia anasema kuwa ni utume mkubwa kwasababu, wao wanabeba misingi ya uumbaji ya Mungu , uhalisia kati ya mume na mke na kizazi cha baadaye, na kazi ya nyumbani inatengeneza masuala kuwa muhimu katika dunia.
Alimalizia katekesi yake akiwasalimu na kuwatakia heri na baraka vijana , wagonjwa , na wanye ndoa. Na kuwataka uvumilivu wote kwa imani ili kukabiliana na mateso , na kwa familia mpya akiwataka wafundishe watoto wao kwa upendo kama Mungu atapenda kuwazawadia .
All the contents on this site are copyrighted ©. |