Baba Mtakatifu Francisko kwa ajili ya maadhimisho
ya Siku 49 ya Kuombea Amani Duniani, 2016, ametangaza kauli mbiu ya ujumbe kuwa :
kushinda tofauti na kushinda amani. Ujumbe unalenga kuondokana na roho ya ubaguzi
wa kujiona kuwa tofauti na mwingine badala yake pamoja na utofauti iwe kujenga moyo
wa amani na wote bila kujali tofauti zilizopo. Hii ni mara ya tatu kwa Papa Francisco
kutoa ujumbe wake kwa siku hii ya Dunia ya kuombea amani tangu alipochaguliwa kuwa
Papa. Papa anaona kwamba, katika wakati huu wetu, hali ya kujali tofauti ni moja
ya sababu za msingi za ukosefu wa amani. Anasema hii tukitazama kwa kina, kutofautiana
mara nyingi, imekuwa ni chimbuko la aina mbalimbali ya ubinafsi, ikisababisha kujitenga,
ujinga, na ubinafsi, kunako leta ukosefu wa uwajibikaji na upendo kwa watu wengine.
Aidha Baba Mtakatifu Francisko anasema, wingi wa habari zinazotolewa juu ya maovu
mbalimbali yanayofanyika duniani, haimanishi uwepo pia wa juhudi nyingi zinazotafuta
kutatua matatizo na changamoto zilizopo, na hasa iwapo habari hizo hazitasaidia kuleta
moyo wa mshikamano uliosimikwa katika misingi ya dhamiri na uwazi . Kwa maana hii,
ni muhimu habari iwe kwa ajili ya kuchangia uelimishaji si tu kwa familia, lakini
kwa makundi mbalimbali ya kijamii, walimu, waandishi wa habari, wasomi na wasanii...hasa
juu ya kila mmoja kuishi kwa uhuru wa dhamiri yake bila kujali tofauti yake na wengine
maana kwa kufanya hivyo huleta ushindi katika kukabiliana na kishawishi cha kutaka
kubagua wengine na kujitenga.
Baraza la Kipapa kwa ajili ya haki na amani, likieleza juu ya Kaulimbiu ya ujumbe
wa Papa kwa Siku ya Kuombea Amani Duninai 2016, linasema Papa Francisko analenga
kusisitiza kwamba, amani haiwezi kupatikana bila Juhudi, au bila ya kuwa na uongofu
kiakili na kiroho, au bila hisia ya ubunifu na ushirikiano katika majadiliano, kwa
faida ya wote.
Kuna hitaji la watu kubadilika kifikra, tena dhatri muhimu na la kidharura, kwa
ajili ya kujenga hisia za uwajibikaji wa kutambua matatizo makubwa na changamoto
za wakati wetu, kama vile, itikadi kali za kutovumilia wengine, kutoona kama kuua
na kutesa wengine kwa sababu ya imani na ukabila, kutokuzingatia uhuru na uharibifu
wa haki za watu wote, unyonyaji wa binadamu na mbalimbali za utumwa, rushwa na uhalifu
wa kupangwa, vita na hatma ya wakimbizi na watu waliolazimishwa kukimbia makazi yao.
Mabadiliko ya moyo na uwajibikaji, haina maana ya kubadili dini au imani kwa kuwa
dini na imani zote za kweli, hudai uadilifu, haki na amani. HIvyo mageuzi ya kuwa
watu adilifu, ni fursa na uwezekano wa kupambana na maovu hayo kwa kuunda utamaduni
wa sheria, ufahamu katika umuhimu wa uwepo wa majadiliano kwa ajili ya kubadilishana
maoni na ushirikiano. Kwa mtazamo huo, pamoja unakuwa ni ujenzi wa msingi thabiti
katika kukabiliana na matatizo na changamoto zinazojitokeza.
Baraza la Kipapa linakumbusha pia kwamba, Ujumbe wa Papa wa kwa ajili ya Siku ya
Kuombea Amani Dunia kwa mwaka huu 2015, pia ulihimiza ujenzi wa amani kwa maisha
ya kila siku , kwa ajili ya kuzishinda changamoto za utofauti, uliosimiskwa katika
mifumo mbalimbali ya utumwa mambo leo. Ujumbe uliotolewa chini ya Mada Mbiu: Hakuna
tena watumwa bali sote ni ndugu kaka na dada. Hivyo tunapaswa kuendelea kujenga uadilifu
na ushirikiano.
Ujumbe unaendelea kusema, Amani huiwezi kuwepo bila haki ya kila binadamu kutambuliwa
na kuheshimiwa kwa mujibu wa uhuru kamili na haki. Ujumbe kwa mwaka 2016 unalenga
kuwa mahali pa kuanzia watu wote wenye mapenzi mema, hasa wale wanaofanya kazi katika
elimu, vyombo vya habari, utamaduni, na kila mmoja kutenda kwa jinsi inavyotakiwa
kwa mujibu wa uvuvio na matazamio ya kujenga umoja na ushirikiano na hivyo kuwa na
dunia iliyo na huru na haki.
Siku ya Kimataifa ya Kuombea Amani Duniani, ilianzishwa na Papa Paulo VI, kwa kila
siku ya kwanza ya mwaka mpya yaani Januari Mosi. Ujumbe Baba Mtakatifu kwa ajili
hiyo, hutumwa kwa Mawaziri wote wanaohusika na Masuala ya nchi za nje duniani, na
pia ujumbe huonyesha mwelekeo wa utendaji wa shughuli za kidiplomasia kwa Jimbo la
Papa katika kipindi cha mwaka mzima.
All the contents on this site are copyrighted ©. |