2015-08-11 15:00:00

Maandamano ya wafuasi wa Jenerali Nshimirimana kufanyika Burundi


Jumapili 9Agosti nchini Burundi ilifanyika maandamano ya wafusi wa Jenerali  Adolphe Nshimirimana wiki moja baada ya kifo chake.

Maandamano hayo yalifanyika katika wilaya ya Kamenge Kaskazini  mwa mji wa Bujumbura.

Inasadikika kufanyika kwa kimya na kwa aina yake ikiwa ni maaandamo ya kwanza kuruhusiwa tangu kuanza kwa machafuko mchini Burundi.

Watu kati ya 1000 na 1500 waliudhuria maandamano hayo wakiwa wamevaa nguo nyeusi na kubeba mishumaa na mabango kama ishara ya kukumbuka Luteri Jenarali Adolphe Nshimirimana aliyekuwa Mkuu wa mzamani wa idara ya Ujasusi.

Hata hivyo uchunguzi wa kifo cha mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi unaendelea kwani Jumapili iliyopita rais Nkurunziza alitoa muda wa wiki moja ili waliohusika na wauaji hayo wawe wamekamatwa badda ya wiki moja.

Ofisi ya mashtaka imetoa wito wa raia wote kutoa taarifa kusaidia kuwapata watu walio husika na mauaji hayo

Aidha taarifa kutoka Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeomba serikali ya Burundi kufanya mazungumzo kwa upya ya amani na vyama vya upinzani kutokana na vurugu zinozotishia nchi. Na nchi ya Ufaransa imeitisha mkutano wa dharura wa mwanachama 15 wa Baraza la kushughulikia vurugu na ghasia kwa nchi hiyo na la Afrika ya kati.

Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki Moon anao mpango wa kutuma ofisa mwandaminzi wa umoja wa Mataifa juu ya nia ya kupunguza kwa haraka migogoro hiyo. Naye  mwanachama wa Baraza kutoka katika nchi ya Nigeria Joy Ogwu  alionyesha wasiwasi  juu ya hali ya kisiasa na usalama nchini Burundi na kuitaka  ianze kwa  haraka ya mazungumzo ya pamoja ili kufikia amani ya kudumu,"








All the contents on this site are copyrighted ©.