2015-08-10 15:49:00

Juba Kanisa lahimiza vyama vinavyopingana kutia sahihi makubaliano ya amani


Makanisa nchini Sudan Kusini yameonyesha kushikamana na pendekezo la mwisho la mkataba wa amani uliotolewa na Kanda ya Mkoa wa Afrika Mashariki pamoja na Mamlaka ya Maendeleo (IGAD), kukomesha vita inayoendelea Sudan Kusini. Pendekezo IGAD la amani,  kama inavyojulikana, kwa sasa linatakiwa kutiwa saini tarehe 17 Agosti, na Rais Kirr upande wa serikali na kiongozi wa upinzani Reik Machar.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa siku nne wa Maaskofu Katoliki katika mji mkuu wa wa Juba, Jumanne iliyopita, Askofu Mkuu wa Juba, Paulino Lukudu Loro, kwa niaba ya Kanisa alitoa  wito kwa pande zinazopigana kutia saini makubaliano hayo. Askofu Mkuu Loro alisema pendekezo IGAD la Amani-Plus pamoja na kwamba si kamili,  lakini ni njia  bora zaidi  kuliko kuendeleza vita, hii iliyozuka upya tangu Desemba 2013.


 








All the contents on this site are copyrighted ©.