2015-08-07 15:35:00

Wimbo Mkuu wa Mwaka Mtakatifu wa Jubilee ya Huruma ya Mungu


Katika ukurasa wa Youtube, Vatican kumechapishwa, Wimbo Mkuu kwa ajili ya maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilee ya Huruma ya Mungu . Kiitikio cha wimbo huo ni :

"Mwenye huruma kama Baba" (chorus)

Na tutoe shukurani kwa  Baba,  kwa kuwa ni mwema ameiumba dunia kwa hekima
Yeye huwaongoza watu wake katika historia; Husamehe na kuwapokea watoto wake

Na tumtolee  shukrani Mwana, Mwanga wa mataifa
Alitupenda kwa moyo wa dhati, 
Toka kwake sisi tunapokea, Na kwake tunajitoa sadaka,
Kwa Moyo wenye hujifunua wazi kwa wale wenye njaa na kiu

Tunaomba kwa Roho Mtakatifu zawadi takatifu saba,
Chanzo cha  kila uzuri, na msaada
Kwa  faraja zake,  tunafarijika kwa
Upendo,  matumaini na stahimili zote.

Tunaomba amani kwa Mungu wa amani zote,Nchi inasubiri Injili ya Ufalme, Neema na furaha,                                                                                         kwake anayependa na kusamehe,itakuwa mbingu na dunia mpya.

Padre Eugenio Costa, Mwanatauhudi na Mwanamuziki, akitoa maelezo juu ya wimbo huu anasema, umeutunga kwa  kuongozwa na Kardinali Rino Fischella, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya uinjilishaji mpya na kwa kushirikiana na Monsinyori Massimo  Palombella, Mwalimu wa Muziki katika Kanisa dogo la Sistine Chapel.

Na kwamba, "kiitikio cha wimbo ni kauli mbiu ya Mwaka wa Huruma ya Mungu, kiini chake ni  kutoka sura ya sita ya Injili ya Mtakatifu Luka, ambapo Yesu anasema: ". Muwe na huruma kama Baba yenu alivyo. 








All the contents on this site are copyrighted ©.