2015-08-06 15:17:00

Sanamu ya Mtakatifu Padre Pio kuwa Vatican wakati wa mwaka wa Jubilee ya Huruma ya Mungu


Kwa muda wa siku nne tarehe 8-14 Februari 2016, wakati wa maadhimisho ya Jubilee ya mwaka wa Huruma ya Mungu, sanamu ya Padre Pio  Pietrelcina, itawekwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro hapa Vatican. Ni maelezo yaliyotolewa na Jimbo Kuu la Manfredonia Vieste San Giovanni Rotondo, na kutoka kwa Shirika la Wakapuchini , Ndugu Wadogo wa Mtakatifu Francis, katika mazingira ya maadhimisho ya mwaka wa Jubilee ya Huruma ya Mungu, kama ilivyotangazwa na Papa Francisco.

Maelezo yao yameonyesha hamu kubwa ya sanamu ya Mtakatifu Padre Pio,  kuwa ndani ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro hapo tarehe 10 Februari , ambayo itakuwa ni Jumatano  ya majivu ambayo pia duniani kote kutatolewa ujumbe wa Utume katika huruma ya Mungu na kwao, itakuwa ni siku maalum ya kupeleka wafuasi wa shirika lao kwenda kuhubiri habari njema na kuungamisha kama ishara wazi hai ya uwepo wa Mtakatifu Padre Pio, katika kuwapokea watu wote katika huruma ya Mungu.

Mtakatifu Padre Pio ni shahidi hai wa huruma ya Mungu kwa watu wateswa na maonevu. Na kwamba uwepo wa sanamu ya Mtakatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro vatican , ni ishara nyeti kwa wote, Wamisionari na  Mapadre, ambamo wanaweza kuchota nguvu mpya za kuwadumisha katika utume wao. Wakifuata mfano wake wa unyenyekevu usiokoma , ukarimu na uvumilivu , unaoonyesha ushuhuda wa kweli kwa huruma ya Mungu Baba 








All the contents on this site are copyrighted ©.