2015-08-05 16:30:00

Upendo wa Papa kwa wahitaji waendelea kuonekana hata wakati wa joto kali


 Askofu Mkuu Konrad Krajewski, msaidizi wa Karibu wa Papa,juu ya upendo wa Papa Francisko kwa maskini,  unaendelea kuonekana bila kudidimia hata katika miezi ya majira ya joto. Huduma mbalimbali za upendo zinaendelea kutolewa katika  majengo mbalimbali ya makazi ya maskini na wasio na makwao. Kama kawaida, watu wa kujitolea, naendelea kutoa chakula kwa watu maskini katika mabwalo husika, vinyoji wakiendelea na huduma ya kunyoa nywele, na wengine kuhakikisha watu hawa maskini wanaburudika na maji baridi na kuoga.

 Askofu Mkuu Konrad yeye mwenyewe ni kati ya watu wa kundi la kujitolea, wanaosaidiana na Masista wa Upendo wa Mama Teresa wa Calcutta, mara kwa mara wakiwa pia na Walinzi wa Papa Kikosi cha the Swiss Guards, wanaosaidia pia kutoa huduma kwa maskini katika maeneo ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Aidha Askofu Mkuu Konrad anaeleza kuwa , yeye na  kundi lake la wasaidizi, kila siku jioni  hutoka na kwenda kugawa maji na chakula katika mabwalo yote yanayotoa huduma ya chakula kwa watu maskini hapa Roma, wakati wa majira ya kiangazi pia. Na muda wote wako mstari wa mbele kwenda kuhudumia mahali popote wanapo hitajika.

Wakati huo huo, taarifa imetolewa kwamba,  mabweni mapya kwa ajili ya makazi ya maskini yanayoandaliwa katika barabara  Via della Conciliazione, karibu yatakamilika na hivyo kutimiza ahadi ya Papa Francisko kaika kuwa karibu na watu maskini, kuwapokea kwa huruma kuu na upendo kamili.








All the contents on this site are copyrighted ©.