Papa Francisko ametuma salaam zake za rambirambi kwa njia ya telegram, kwa Kardinali
Donald Wuel wa Jimbo Kuu la Washington, Marekani, kufuatia kifo cha Kardinali William
Wakefield Baum. Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Washington.Katika salam hizo za
rambirambi, Baba Mtakatifu Francisko ameonyesha masikitiko yake ya dhati, na kusema
kupitia sala na maombi, atakuwa karibu na wote walio waliotiwa simanzi na kifo hiki,
na kwa waamini wote wa Jimbo Kuu la Washington. Na pia ameonyesha shukrani zake za
dhati kwa huduma ya Kardinali Baum kwa Kanisa na hasa kwa kazi ya kuliongoza jimbo
kuu la Washington, na utendaji mwingine mbalimbali katika majukumu na Kanisa na Vatican.
Papa amesema , anaungana na Kardinali Wuerl, kuiombea roho ya marehemu Kardinali
Baum, huruma ya Mungu Baba. Na wote watakaoshiriki katika Ibada ya Misa ya Wafu
na maziko na wote wanaoombeleza kifo hiki , wajaliwe tumaini ka Kristo Mfufuka. Kwao
wote Papa amewapa Baraza zake kama ahadi ya nguvu na faraja katika Bwana. Mwadhama Kardinali William Wakefield Baum, Askofu Mstaafu Washington, alifariki
siku ya Ijumaa tarehe 24 Julai 2015, akiwa na umri wa miaka 80. Kwa kifo chake, Vatican imesema, Baraza la Makardinali limebaki na Makardinali
220, kukiwa na wenye haki ya kupiga kura 120 na wasiokuwa na haki 100.
All the contents on this site are copyrighted ©. |