Jimbo la Papa kwa mara ingine limerudia kutoa upya wito wake, unaodai ushirikiano wa kimataifa , kwa lengo la kusitisha uhasama wa vita na migogoro katika Mashariki ya Kati na kusaidia mamilioni ya wakimbizi kutoka Iraq na Syria kwa huduma za ubinadamu.
Alhamisi wiki hii, katika hotuba yake katika mjadala wazi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya, "Hali katika Mashariki ya Kati, ikiwa ni pamoja na Palestina” Askofu Mkuu Bernard Auza, Mjumbe wa Kitume wa Papa na Katibu Mtazamaji wa Jimbo Takatifu katika Umoja wa Mataifa, aliitaja hali ya ubinadamu katika eneo la Mashariki ya kati ni mbaya hasa Syria na Iraki kwamba inatia wasiwasi.
Amesema, dhamira zinadai kufanya upya kila jitihada na mbinu kwa ajili ya kupata ufumbuzi kaiika mgororo huu wa kisiasa unaorarua maisha ya watu Syria. Hawawezi kuendelea kuwa watazamaji tu wasiokuwa na lolote la kufanya katika uhalifu huu au kujiweka pembeni wakati mataifa hayo yana haribiwa.
Askofu Mkuu Auza ameeleza na kutaja jinsi mataifa jirani kama Lebanon na Yordani yanavyolemewa na wingi wa wakimbizi na hofu zinazotokana na kikundi cha kigaidi cha Isis, akitaja haja ya uwepo wa mshikamano wa dunia, kupata ufumbuzi katika mgogoro huu. .
Na kwamba jimbo Takatifu linaendelea kufuatilia kwa ukaribu hali ya ubinadamu katika Mashariki ya Kati, ambayo inateswa vikali na mizozo inayopanuka siku hadi siku. Na kwa bahati mbaya, jumuiya ya kimataifa, sasa inaona kama jambo la kawaida kaika nchi za Mashariki ya kati kuwa na migogoro kama hiyo. Inasikitisha kuona mpaka sasa hapajafanikiwa kupata ufumbuzi muafaka kwa tatizo hilo.
Hasa wasiwasi mkubwa ni jinsi hali ya ubinadamu inavyo athirika kwa wengi. Mateso ya watu wema katika taifa hilo yanadeai kufanya kwa upya dhamira ya jumuiya ya kimataifa, kutafuta ufumbuzi wa kisiasa kwa mgogoro huo.
Askofu Mkuu Auza alionya katika mjadala huo kwamba hawapaswi kuendelea kuwa watazamaji wasiokuwa na msaada. Kuwa pembeni wakati nchi hiyo inazidi kuharibiwa. Hali nchini Syria inahitaji jumuiya ya kimataifa kuweka kando maslahi ya mengine na kutoa kipaumbele kwa taifa hilo kwa lengo la kuokoa maisha ya wengi , yanayo angamizwa kila siku, katika vita hiyo ya wenyewe kwa wenyewe
Jimbo la Papa , linasema kama Papa Francisco alivyosema wakati wa hija yake katika
Nchi Takatifu mwaka jana: "Wakati umefika kwa kila mtu kupata ujasiri wa kuwa mkarimu
na mbunifu katika huduma kwa manufaa ya wote, ujasiri wenye kulenga kutengeneza
amani katika maoni kwamba, kila mtu anayo haki ya kuishi katika nchi hiyo kwa amani
na usalama wenye kuzingatia maagizo na maamuzi yanayotambuliwa na wengi, yaani Uumoja
wa Mataifa. Katika hali hii, ujumbe Jimbo la Papa, ulisisitiza mchakato wa amani
usonge mbele kama nguvu na jawabu pekee ya kufanikisha amani na utulivu kwa taifa
la Syria na Iraki, kwa msaada wa jumuiya ya kimataifa.
All the contents on this site are copyrighted ©. |