Papa Francisko kwa pamoja na Mameya wa Majiji kadhaa waliweka saini zao katika hati yenye azimio lao la pamoja linalolenga kupambana na uharibifu wa mazingira na biashara haramu ya binadamu. Hati hiyo iliyotiwa saini, ni matokeo ya mkutano wao wa siku mbili, mjini Vatican, uliohudhuriwa na Papa na Mameya, kutafakari pamoja kwa kina, juu ya mafanikio ya watu na sayari yetu, hasa wakilenga juu ya mabadiliko ya tabianchi na wimbi la biashara haramu ya watu. Utiaji wa saini ulifanyika katika ukumbi mpya wa sinodi wa mjini Vatican, kama inavyoelezwa katika tovuti ya Vatican: www.pass.va
Mkutano huu wa tarehe 21-22, uliandaliwa na Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya elimu ya Sayansi na Sayansi ya Jamii, kutafakari umuhimu wa mshikamano katika kupambana na dharura kuu mbili: Mabadiliko ya tabia nchi yanayosababishwa na utendaji mbovu wa binadamu ikiwemo hali ya hewa , pili ubaguzi wa kijamii wenye kusababisha umaskini wa kukithiri, unaokuwa mtego kwa watu kuingizwa katika biashara haramu ya binadamu na utumwa mambo leo na uhamiaji wa kulazimishwa kutokana na hali mbovu kimaisha.
Washiriki wa Mkutano huu, wanakiri katika azimio lao kwamba, wakiwa wameungana
pamoja katika warsha hii, toka pande mbalimbali wenye tamaduni na njia mbalimbali
za maisha, kwa pamoja wameketi kutafakari shauku ya binadamu kwa ajili mafanikio,
haki na mazingira endelevu amani, furaha ya kuishi.
Na kwamba katika nafasi hii msingi kimaadili, miji inakuwa na jukumu kubwa na muhimu,
katika kuhakikisha watu wote licha ya maisha yao kutofautiana kimila na kitamaduni,
wote wanapaswa kuzingatia heshima kwa mambo ya asili na viumbe kama wajibu wa kijamii,
na wa kila mtu binafsi na mahusiano yake kwa manufaa ya watu wote. Na wanathibitisha
uzuri wa ajabu na wema asilia wa ulimwengu katika asili yake, inayopaswa kutambuliwa
kuwa ni zawadi ya thamani sana aliyokabidhiwa binadamu kwa ajili ya manufaa ya maisha
yake ya kila siku. Na hivyo unakuwa ni wajibu kwa kila binadamu, kimaadili kuwa
mtetezi na si mharibifu wa bustani hii , ambayo ni makazi na nyumbani kwa viumbe wote.
Pia azimio limekiri kwamba, mabadiliko ya tabianchi yanayo sababishwa binadamu, ni ukweli wa kisayansi, hivyo kunahitajika udhibiti madhubuti kama jambo muhimu katika uadilifu wa ubinadamu.
Na licha ya kwamba hawahusiki sana na uharibifu wa hali ya hewa , watu maskini
na waliowekwa pembezoni mwa Maendeleo, ndiyo wanapambana zaidi na kitisho cha mabadiliko
ya tabianchi kutokana na utendaji mbovu wa binadamu , na hivyo kusababihs uwepo wa
ukame wa mara kwa mara, vibunga na tufani kali joto la hewa kupanda na kiwango cha
waji ya bahari kuongezeka.
Azimio limeonyesha kujali kwamba wanaoathirika zaidi na utendaji huu mbovu wa binadamu.
Na kwamba, leo binadamu ana vyombo vya hali ya juu kiteknolojia,akiwa pia amesheheneza
rasilimali fedha na ufahamu wa kutosha jinsi anavyoweza fanya mabadiliko katika
tabia nchi hasa hali ya hewa , na pia ujuzi wa kutosha katika kukomesha umaskini uliokithiri,
kwa kutumia mikakati mbinu kwa ajili ya ufumbuzi maendeleo endelevu, ikiwa ni pamoja
na kupitishwa kwa mifumo ya nishati yenye kuzalisha hewa kidogo ya ukaa (kaboni) ikishamirishwa
na utoaji wa habari na teknolojia katika mawasiliano.
Azimio linaendelea kuzungumzia ufadhili wa maendeleo endelevu, ikiwa ni pamoja na udhibiti madhubuti wa mabadiliko ya tabia nchi binadamu akitakiwa lazima kuimarisha njia mpya, katika kipindi cha mpito kuelekea uzalishaji wa hewa kidogo ya ukaa kwa kuwa na nishati mbadala, na kwa njia ya harakati zenye kuzingatia amani, ambazo zinaweza pia leta mabadiliko katika mifumo fedha ya umma kutoka matumizi makubwa ya kijeshi na kuingia haraka katika uwekezaji kwa ajili ya maendeleo endelevu.
Na dunia inatakiwa kuona kwamba, Mkutano wa kilele utakaofanyika Paris baadaye mwaka huu (COP21) kama nafasi nzuri ya mwisho kujadili mipango hiyo ya utendaji wa binadamu, uwezeshe joto libaki chini ya 2 ° C kwa ajili ya usalama wa binadamu na viumbe, katika maono kwamba kuna hatari ya joto kupanda kwa nyuzi zote 4 C°na hata zaidi .Hivyo Viongozi wa kisiasa na wanachama wote wa Umoja wa Mataifa na nchi wanachama, wana wajibu maalum katika mkutano huu wa COP21 kufikia makubaliano thabiti na jasiri kwa ajili ya kupambana na ongezeko la joto duniani, libaki katika ukomo wa usalama kwa binadamu, na kulinda maskini na wanaoishi katika mazingira magumu kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayoendelea kuathiri maisha ya watu maskini na kuwekwa hatarini. Ni lazima nchi zenye kipato kikubwa kusaidia kufadhili gharama zinazo tokana na mabadiliko ya hali ya hewa katika nchi za kipato cha chini, kama maamuzi ya nyuma yalivyokwisha fanywa na nchi i zenye kipato kikubwa.
Mabadiliko ya hali ya hewa , yanahitaji kukabiliana kwa haraka kwa dunia kuwa na
uzalishaji mdogo wa hewa ya kaboni kwa kutumia mbadala mingine katika vyanzo vya nishati
na usimamizi endelevu wa mazingira. Mabadiliko haya Lazima yafanywe katika mazingira
ya Malengo ya maendeleo endelevu, kama itakavyo kubaliwa kimataifa, sambamba na kukomesha
umaskini uliokithiri; kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya, elimu bora, maji
safi na salama, na nishati endelevu; na kushirikiana ili kumaliza biashara ya binadamu
na aina zote za utumwa wa kisasa.
Kama madiwani wameahidi katika miji yao na makazi ya mijini, kuwawezesha wale wote
watakao kosa ajira na wale wanaoishi katika mazingira magumu kutokana makubaliano
y akupunguza uzalishaji wa hewa ya kaboni, na matukio mengine yanayohusiana na masuala
mengine yanayohusiana kiuchumi, kijamii na kimazingira, kama majanga na maafa, ambayo
huwa na mwelekeo wa kuendeleza biashara haramu ya binadamu na hatari za wahamiaji
wa kulazimishwa.
Wakati huo huo, Madiwani wameahidi kusitisha katika hali zote matendo unyanyasaji,
unyonyaji, biashara haramu na aina zote za utumwa wa kisasa, ambayo ni uhalifu dhidi
ya ubinadamu, ikiwa ni pamoja na kazi za kulazimishwa na ukahaba, ulanguzi, na utumwa
wa ndani kwa kuendeleza maendeleo endelevu kitaifa yenye kuunganisha mipango ya kijamii
ikiwemo kutoka makazi kwa wanyonge, na kujiepusha na kishawishi cha kuwarejesha wahamiaji
kwa nguvu makwao
Mameya wa miji wanataka miji yao iwe ni makazi ya mazuri kwa ustawi wa watu, umoja na mshikamano wa kijamii, mahali pa salama, ushujaa na endelevu . Wanadai kila Sekta na wadau wote lazima kufanya Sehemu yao, nao wana ahadi kutenda katika uwezo wao kama mameya na kama madiwani na watu binafsi..
All the contents on this site are copyrighted ©. |