Adhimisho la miaka mia tano, alipozaliwa Mtakatifu Philipo Neri, linakumbusha kwamba mchungaji mwema hukaa karibu na kondoo wake. Ni ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisco, kwa ajili adhimisho la miaka mia tano ya kuzaliwa Philipo Neri , hapo tarehe 21 Julai 1515.
Mama Kanisa, hasa kwa namna ya kipekee katika Jimbo la Roma, Jumanne hii, ameadhimisha Siku kuu ya kuzaliwa Mtakatifu Philip Neri , Mtakatifu Maarufu aliyezaliwa Florence Italia, 21 Julai 1515, na baadaye kuhamia Roma, ambako alikuwa na maisha kustajabisha, yenye upendo mkuu kwa watu maskini zaidi.
Papa Francisco anasema ingawa zimepita karne tano , kumbukumbu za uwepo wake zinaendelea kuwa hai miongo mwa watu wa Roma, , hasa kwa jinsi alivyoishi kwa mshikamano na kwa furaha kubwa na maskini na leo anaendelea kuwa harufu nzuri inayovutia kutumikia maskini, kama inavyo endelezwa na Shirika lake la Mtakatifu Philipo Neri .
Kwa ajili ya Siku Kuu hii, Papa Francisco kwa roho ya Kibaba, hapo Mei 26 alipeleka barua kwa Shirika la Mtakatifu Phillipo Neri , kwa ajili ya kuadhimisha miaka mia tano tangu kuzaliwa Philip Neri.
Papa katika Ujumbe wake, ameonyesha kutambua jinsi Mitume Petro na Paulo, na Philip, wanavyo tambuliwa na kuheshimiwa kama Mitume watatu wa Roma, kutokana na mapenzi yao kwa watu wa Roma. Wakazi wa Roma husema , Philip Neri ingawa alizaliwa wa Florence, alizaliwa upya Rome, kwa ajili ya watu wa Roma. Papa amerejea maelezo ya kihistoria yanayosema, alifahamika kote katika maeneo ya wazi ya jiji na katika vichochoro vya Roma, ambako waliishi watu maskini zaidi. Philipo aliwatembelea watu hao kama mchungaji Mwema bila ya kujali hali yao duni, yeye aliisikia harufu ya kondoo na siyo harufu mbaya ya maradhi na umaskini. Aliwafariji kwa utajiri wake wa kiroho.
Ujumbe wa Papa Francisco unaendelea kuyakumbuka maisha ya ukarimu na upendo wa
Mtakatifu Philipo Neri, hasa kwa jinsi alivyo kuwa pia na mapenzi ya Neno la Mungu
. Papa anasema hii ilikuwa ni siri yake iliyompa nguvu na ujasiri wa roho. Ubaba
wake wa kiroho, anaendelea kusema Papa Francisko, uliangazia mapito ya kazi yake
yote, sifa na uaminifu kwa watu na katika furaha ya uongofu unaotokana na imani
thabiti , neema isiyoondoa asili, lakini hujaza nguvu na ukamilifu. Ndiyo yeye
aliwaendea waliokuwa dhaifu na kuwapa kidogo alichokuwa nacho, na wote walimkaribia
na kuwa marafiki zake, Maelezo binafsi ya Mtakatifu Philipo Neri yanasema. Na kwamba,
kwa hiari alitenda na kujikatalia mambo ya mpito ya kidunia, akipendelea zaidi kujifurahisha
na kujielimisha na fadhila za Ukristo , wakati huo huo, akiwa mtu wa nidhamu na
mapenzi makubwa katika utume wake na katika kumkubali Kristo kama ukweli wa maisha
yake. .
Papa Francisco ameeleza na kutoa Shukrani zake za dhati kwa utume wa Mtakatifu Philip,
akionyesha pia kutambua ahadi ya wokovu wa roho kuwa kipaumbele kwa ajili ya Kanisa,
akisema, hii ndiyo njia, wanayo paswa kutembea ndani yake wachungaji wote wa Kiroho,
katika kuwaongoza na kusaidia watu kufikia ukomavu wa imani yao. Kuwa mchungaji
mwenye ni kuitoa nafsi kwa ajili ya wengine, kama Philipo , ambaye mwaka 1551, alijiunga
katika daraja la ukuhani bila kubadilisha mtindo wa maisha yake. Katika kumbukumbu
za nyakati, sura yake haijafutika machoni pa jamii. Kutokana na mapenzi yake kwa jamii
iliyokuwa mzunguka, iliundwa jumuiya ya kwanza kwa karama za sura yake , ambayo
mwaka 1575 ilipokelewa kwa ridhaa ya Papa Gregory XIII.
Padre Philipo Neri , anaendelea kukumbukwa, jinsi daima alihimiza waamini , kuwa
wanyenyekevu, kujishusha chini kwa unyenyekevu, kama watoto wa Mungu. Aliwaonya kwamba,
katika kuwa watoto wa Mungu "haitoshi kuwa watu wa kuheshimu yaliyo ya juu peke yake
lakini pia ku heshimu yote yaliyoumbwa na Mungu.
Papa Francisco ameutaja huo kuwa ndiyo wosia msingi wa Mtakatifu Philip, kuwa na unyenyekevu kama wa mama Bikira Maria alivyokuwa miguuni pa Yesu.
Mtakatifu Philip Neri , Mtume wa tatu wa Roma, alifumba macho yake daima Mei 26, 1595. Lakini upendo wake kwamwe haujazima katika mioyo ya watu Roma, ambao kwa wakati huu Papa Francisko anatumaini wanajiandaa vyema pia kwa ajili ya Jubilee ya Huruma ya Mungu. Anasema huu si muda wa kulala, kwa kuwa Paradiso haikujengwa kwa ajili ya wazembe.
All the contents on this site are copyrighted ©. |