Papa Francisko ametaja maneno matatu : kutazama , huruma na kufundisha kuwa tabia ya kiongozi yoyote mwema. Papa alieleza hilo wakati wa sala ya Malaika wa Bwana akiwa hapa Vatican, ambako makumi ya maelfu ya watu walikusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, majira ya adhuhuri kumsikiliza licha ya jua kali.
Hotuba ya Papa ililenga katika somo la Injili ya Jumapili hii ambamo mnaeleza kwamba, Mitume, baada ya kufanya kazi nyingi kwa furaha lakini pia walionekana kuwa na uchovu, wakihitaji kupumzika kidogo kando faraghani, mbali na makundi ya watu na Yesu alitambua hilo. Lakini watu walivyoona hivyo, waliwatangulia mbele yao. Yesu aliwatazama watu hao na kuwahurumia akiwaona kama wanakondoo wasiokuwa na mchungaji, hivyo alianza kuwa fundisha mambo mengi( Rej. Mk6,31-34).
Baba Mtakatifu Francisko anasema katika somo hili, tunajifunza mambo matatu :
kuona kwa makini, kuwa na huruma na kufundisha. Mambo haya , ni sifa ya kiongozi au
mchungaji mwema. Papa anafafanua sifa ya kwanza na ya pili, katika mtazamo wa mahusiano
yake na Yesu,akisemani kutazama mambo kwa makini si kama mtalaam wa sosholojia au
mwanahabari au mpiga picha, lakini ni kutazama katika kina cha moyo,mtazamo wa "macho
ya kiroho". Hivi vitenzi viwili,kuona na huruma, ni sifa ya mchungaji mwema kama
Yesu alivyo. Papa aliendelea kutazama kwa kina huruma ya Yesu akisema, haikuwa
hisia za kibinadamu, lakini hisia halisi za Masiya aliye alifanyika mwili, ambaye
ni huruma ya Mungu. Na huruma hii, ilimpa Yesu hamu ya kulisha umati kwa chakula
cha Neno lake kwa kufundisha.
Baada ya kutafakari ujumbe wa Injili, Papa pia aliutumia wakati huu wa sala ya Malaika
wa Bwana kutoa shukurani zake kwa Roho wa Yesu, Mchungaji Mwema, kwa kumwongoza
wakati wote wa ziara yake ya kitume ya zaidi ya wiki, kutembelea Mataifa matatu ya
Amerika ya Kusini Ecuador, Bolivia na Paraguay hivi karibuni. Mbele ya mahujaji na
wageni, Papa kwa dhati amemshukuru Mungu kwa ajili ya zawadi hii. Na pia alirudia
kwa mara ingine kutoka shukurani zake kwa mamlaka ya nchi hizo kwa ukarimu wao na
ushirikiano. Na kwa upendo mkubwa, amewashukuru tena ndugu zake Maaskofu, mapadre,
watawa, walioweka maisha wakfu na watu wote kwa ajili ya mapokezi mazuri na ushiriki
wao. Kwa ajili hiyo Papa alimtukuza Bwana aliyefanikisha kazi za utume wake kwa Watu
hawa Mungu, walio katika hija ya maisha, wakiwa wamehamasika katika imani na katika
utamaduni wao. Na kwa ajili ya kuwawezesha wote kumtukuza Mungu kwa shukurani na
sifa kwa ajili ya mazingira asilia mazuri, yenye utajiri mkubwa nchi hizo.
Papa amekiri kwamba bara hili la Amerika ya Kusini , lina utajiri mkubwa wa ubinadamu na uwezo wa kiroho, uliofumbatwa katika thamani ya kina cha mizizi ya maadili ya Kikristo, licha pia ya kukabiliwa na matatizo makubwa ya kijamii na kiuchumi. Kwa ajili ya kutoa mchango wake katika kupata ufumbuzi wa changamoto zinazo wakabili, amesema jukumu la Kanisa, kuendelea kuhamasisha tunu za kiroho na kimaadili katika jamii, kwa kushirikiana na watendaji wengine wote kwa ajili ya kujenga ustawi wa jamii nzima..
Na ameonyesha kutambua jinsi wanavyokabiliwa na changamoto kubwa katika kuitangaza
Injili ya Kristo, mbele ya uso huo, Papa anatoa mwaliko kwa wote kuteka toka kwa
Kristo Bwana neema zake, kwa kuwa neema za Bwana zina nguvu kubwa ya kuokoa na ni
nguvu ya dhamira ya kumshuhudia Kikristo, katika kukuza usambazaji wa Neno la Mungu,
hadi roho wa kidini aweze kuwa nguvu zaidi kwa watu wote, na katika kuwa daima
shahidi aminifu wa Injili.
Papa Francisco alieleza na kuomba maombezi ya Mama Yetu Maria wa Guadalupe, , ili
kwamba, wote wa Amerika ya Kusini, waweze kuheshimu kuwa chini ya Msimamizi wao Mama
Yetu wa Guadalupe. Pia Papa ameyakabidhi matunda yote ya ziara yake ya kitume Amerikaya
Kusini, katika Usimamizi wa Maria, na ameitaja ziara hiyo kwamba hataisahau.
All the contents on this site are copyrighted ©. |