2015-07-14 13:45:00

Mkutano wa Kimataifa wa Tatu juu ya ufadhili wa Fedha katika Maendeleo ya Dunia


Tangu Jumatatu hii 13-16 Julai 2015, mjini Addis Ababa, Ethiopia, kunafanyika Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa Fedha  kwa ajili ya Maendeleo endelevu. Mkutano unaohudhuriwa na wawakilishi wa ngazi ya juu wa kisiasa, Wakuu wa Nchi na Serikali, na Mawaziri wa Fedha, Mawaziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano,  pamoja na wadau wote muhimu kutoka  taasisi na  asasi zisizo za kiserikali na sekta ya biashara kaika mashirika makubwa.  Mkutano huu  unatazamiwa kutengeneza uwanja wa majadiliano kati ya serikali za nchi na kukubaliana uwepo wa  matokeo yanayoweza kuanzisha mchango muhimu na kusaidia utekelezaji wa ajenda za baada ya malengo ya maendeleo ya 2015.

Mkutano huu unafanyika katika mtazamo wa yaliyomo katika maazimio ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kipengere namba  68/204 na 68/279, na unalenga katika :
 Kutathimini mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Makubaliano ya kifedha , Azimio la Doha, utambuzi wa  vikwazo vilivyojitokeza katika kufanikisha malengo na madhumuni  waliyokubaliana awali, ikiwa ni pamoja na utendaji na juhudi zilizolenga  kushinda vikwazo hivyo.

Pili ni kujali masuala mapya na yanayojitokeza, ikiwa pia katika mazingira ya Juhudi za hivi karibuni za kimataifa katika kuboresha ushirikiano wa maendeleo ya kimataifa   katika masuala yote yanayohusika na ushirikiano wa kimataifa katika maendeleo. Utendaji katika mwingiliano wa vyanzo vyote vya fedha za maendeleo, umoja kati ya malengo fedha katika vipimo vitatu vya maendeleo endelevu; na
haja ya kuunga mkono ajenda ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa baada ya malengo ya  2015..

Tatu ni Kuhamasisha na kuimarisha mfumo wa  fedha kwa ajili ya ufuatiliaji wa mchakato wa maendeleo endelevu.

Taarifa inasema, kazi za maandalizi ya serikali kwa ajili ya mchakato wa Mkutano huu unafanyika , zilizinduliwa tarehe 17 Oktoba 2014, ikifuatiwa na vikao  mfululizo rasmi na isiyo rasmi,  mikutano iliyo shirikisha  vyama vya kiraia na sekta ya biashara hadi Machi 2015, ikiwa ni pamoja na vikao vya kuandaa hati ya matokeo, kazi iliyofanyika  mwezi Januari, Aprili na Juni 2015.

Katibu Mkuu  wa Umoja wa Mataifa,  Bwana Ban Ki Moon, Jumapili akihutubia vikundi vya wawakilishi wanaoshiriki katika Mkutano huu, alitaja wajibu wa vyama vyakiraia katia kufadhiliwa maendeleo na kwamba vyama vya kiraia duniani kote vina wajibu w akushikiza serikali na sekta ya biashara kuhakikisha uwekezaji wa muda mrefu na endelevu. Mkutano wa Jumapili uliandaliwa kama hafla ya kuwakaribisha wajumbe wa Mkutano huu wa kimataifa wa Tatu  juu ya ufadhili wa Fedha katika maendeleo endelevu, mkutano uliofunguliwa  Jumatatu hii.

Bwana Ban, alishukuru vyama  na mashirika ya kiraia, kwa ushiriki na Utetezi  na Juhudi  zao katika nchi , kwa ajili ya kusukuma mbele maoni kamambe juu ya ajenda ya ufadhili katika maendeleo akisema,  vyama vya kiraia na Mashirika ya kujitegemea  wana jukumu muhimu la kuiwajibisha  Serikali  kugharamia ajenda za baada ya malengo ya maendeleo ya 2015. Hotuba ya Katibu Mkuu ilitaja maeneo manne, ambamo  asasi za kiraia zinaweza cheza: kwanza,  uhamasishaji wa rasilimali, katika mtazamo wa kuboresha ushirikiano wa kimataifa katika masuala ya kodi. Pili, nchi wafadhili wanahitaji kutimiza ahadi zao juu ya Misaada ya Maendeleo rasmi ikiwa ni pamoja na fedha ya hali ya hewa. Tatu, wingi wa uwekezaji binafsi kama jambo muhimu. Hatimaye alisisitiza juu ya umuhimu wa kuzingatia biashara, madeni na masuala ya utaratibu wazi zaidi katika  mtiririko wa fedha.








All the contents on this site are copyrighted ©.