Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa jioni aliingia nchini Paraguay, sehemu ya mwisho ya ziara yake ndefu ya kitume , kutembelea mataifa matatu ya Amerika ya Kusini, kama mhujaji na shahidi wa Habari Njema ya Upendo wa Kristo kwa watu wote.
Pamoja na hali mbaya ya hewa , Papa alipokelewa kwa shangwe zote kitaifa. Mara baada ya hafla fupi ya mapokezi katika uwanja wa Kimataifa wa Asuncion wa Paraguay, ambako watoto walimpamba kwa shada la maua kwa utamaduni wao, kwa muda mfupi alipumzika katika chumba kilichokuwa kimeandaliwa akiwa na mwenyeji wake Rais Horacio Manuel Cartes Jara, na baadaye kwenda Ikulu, ambako maofisa wa ngazi ya juu katika serikali ya Paraguay walitambulishwa kwake. Akiwa Ikulu pia alibadilishana zawadi na mwenyeji wake.
Baadaye Papa akiwa katika viwanja vya Ikulu, aliwahutubia viongozi wa serikali
na wanasiasa ambamo alianza kwa kutoa shukurani kwa mapokezi mazuri na kwa ukarimu
wao. Lakini mara alikumbuka uchungu historia ya Paraguay kati ya '800 na' 900 ambayo
ilikuwa ni miaka ya mateso ya kutisha ya vita, migawanyiko, ukosefu wa uhuru na ukiukaji
wa haki za binadamu.
Alikitaja kipindi hicho kwamba ilikuwa ni wakati wa uchungu mkuu na vifo vya kutisha.
Lakini basi baadaye ushindi uliweza kupatikana kwa kujenga tena moyo wa mshikamano
kwa watu Paraguay,na hivyo kuzishinda taabu nyingi na mateso na kuendelea ujenzi
wa taifa, jitihada zilizo letea taifa amani na mafanikio.
Aliendelea kuzungumzia migogoro ya zamani na nchi nyingine za Amerika Kusini, na
kutoa shukurani na pongezi kwa wanawake wa Paraguay ambao, waliweza simama imara
katika kutoa jibu la kusitisha mauaji ya watu wao, katika vita hivyo vya dhuluma,
vilivyofanya maafa na uharibifu makubwa kwa watu wa taifa hilo. Papa kwa masikitiko
aliendelea kujali jinsi mabegani mwao, hao akina mama, wake na wajane walivyotenda
kwa ujasiri mkubwa na kuweza kuendeleza familia zao na nchi yao, na kurejesha katika
kizazi cha vijana matumaini bora kwa siku za baadaye . Papa alieleza na kuwaombea
Baraka za Mungu wanawake wa Paraguay, taifa tukufu sana Amerika ya Kusini.
Papa akiendelea kuutazama uchungu na madhara ya vita, na kukemea mawazo yote yanayoweza
zua vita akisema , kamwe pasiwe na vita na madhulumu dhidi ya haki na hisia zote
za kutaka kulipiza kisasi na chuki na upuuzi wote wa vita. Pasiwe tena kinyongo
na chuki na kati ya ndugu! Daima, kizazi hiki chetu na cha baadaye iwe ni kujenga
amani zaidi! Amani siku hadi siku. Amani katika maisha ya kila siku, kwa watu wote
iwe hivyo. , Daima na iwe kuepuka vishawishi vyote vya kujenga kiburi, maneno ya
kukera na ufedhuli. Badala yake na iwe kuendeleza ufahamu kupitia njia ya mazungumzo
na ushirikiano.
Hotuba ya Papa iliendelea kuutaka uongozi wa kiserikali na wanasiasa na watu wote
, kutoa kipaumbele kwa maskini, kama ambavyo imekuwa sifa ya taifa la Paraguay kwa
muda wa miaka kadhaa, kuendeleza nia ya kujenga demokrasia imara, kupambana na rushwa,
na kuhamasisha miundo na taasisi imara za kidemokrasia. Papa amehimiza kuepuka majaribu
yoyote yanayotaka kumomonyoa demokrasia rasmi. Pia amehimiza uimarishaji wa majadiliano
kama njia pekee ya kukuza manufaa ya wote, kwa kuzingatia utamaduni wa kuheshimiana
, na utambuzi wa tofauti halali na maoni ya wengine, kama njia ya kuondokana na migogoro
na mgawanyiko wa kiitikadi.
Papa amesema "hadhi ya wanyonge ni kipimo cha mfumo wa kiuchumi!” Na kwamba, ni lazima kuheshimu utu wa binadamu, hasa wanaoishi katika mazingira magumu zaidi na wasioweza jitetea Papa ameonyesha kufurahia ushirikiano wa Kanisa Katoliki kwa taasisi zinazo tetea haki na umoja wa kijamii, akisema huo ni mwanga unaomulika njia ya huruma wazi ya Kristo kwa watu wote. Na kutenda kwa haki, hujenga upendo ulio imara zaidi kati ya mtu na mtu , na hivyo kufuta moyoni chuki na wivu usiokuwa na maana. Na hakuna anayeachwa nje au kupuuzwa katika mipango yote ya Kijamii, Papa amesisitizia watawala na wasiasa Paraguay.
All the contents on this site are copyrighted ©. |