Jumapili 5 Julai 2015, Baba Mtakatifu Francisco majira ya asubuhi alianza ziara ya kitume kwa nia ya kutembelea mataifa matatu ya Amerika ya Kusini , Ecuador, Bolivia na Paraguay kama shahidi wa Injili. Ziara inayomchukua muda wa siku tisa, hadi tarehe 13 Julai atakaporejea Roma.
Jumatatu 6 Julai , Papa akiendelea na ziara hii katika siku ya Pili, ana ratiba ya matukio mawili makubwa kwanza itakuwa ni kuongoza Ibada ya Misa katika uwanja wa Guayaguil majira ya saa tano kwa saa za Ecuador , ambayo ni majira ya jioni kwa saa za Afrika Mashariki. Na baadaye majira ya jioni kwa saa za Ecuador, Papa atakutana na umma wa Ecuador katika Kanisa Kuu la mjini Quito.
Hapo siku ya Jumapili, Papa Francisco , mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Marisal Sucre Quito Ecuador , baada ya kusafiri mwendo wa kilomita 10,103 kwa muda wa saa 13 hewani kwa ndege ya Altalia, alilakiwa na wenyeji wa Ecuador wakiongozwa na Nuncio wa Papa Ecuador, AskofuMkuu Giacomo G. Ottonello, Askofu wa Jina wa Sasabe,na Rais wa Ecuador Raffael Correa, ikifuatiwa hafla fupi ya makaribisho.
Mahali hapo, Papa kwa heshima na taadhima alitoa hotuba yake fupi, ambamo , alishukuru kwa majaliwa yake Mungu yaliyo mwezesha tena kurudi Amerika ya Kusini, kuwa tena pamoja na watu wa taifa zuri la Ecuador. Na alikiri kujisikia furaha na kushukuru kwa joto joto la makaribisho mazuri, akisema ni ishara ya ukarimu na wema wa watu wa Ecuador.
Na kwa namna ya kipekee alitoa shukurani zake kwa Rais Raffael , na viongozi katika mamlaka serikalini , pamoja na ndugu zake katika dekania ya maaskofu, waaminifu wa Kanisa nchini Ecuador, na wale wote ambao wameweza kuifunua mioyo na nyumba na taifa lao kwa ukarimu, kwake yeye Papa na wote alioandamana nao.Papa alionyesha kuthamini na kutoa shukurani za dhati.
Aliendelea kusema, licha kwamba siku za nyuma alitembelea taifa hilo kwa mara kadhaa
kwa sababu za kichungaji, katika ziara hii amekwenda kama shahidi wa huruma ya Mungu
na imani katika Yesu Kristo.Papa alishuhudia jinsi kwa karne na karne, imani kwa
Kristo , imeweza tengeneza umbo la utambulisho wa Wakristo katika taifa la Ecuador
na kuzaa matunda mengi mazuri, wakiwemo Mtakatifu Mariana de Yesu, Mtakatifu Miguel
Febres, Mtakatifu Narcisa de Jesús na Mwenye Heri Mercedes de Jesús Molina, aliyetajwa
kuwa Mwenye Heri huko Guayaquil miaka thelathini iliyopita, wakati wa ziara ya Papa
Yohane Paulo II. Hawa, kama ilivyo na wengine kama wao, waliishi imani yao kwa nguvu
na shauku, na kwa matendo yao ya huruma wao wamechangia kwa njia mbalimbali , kuboresha
jamii Ecuador katika siku zao.
Papa kisha aliugeukia wakati wetu akisema, katika wakati wetu wenyewe pia, tunaweza
kupata katika Injili, ufunguo wa kukabiliana na changamoto za kisasa, kuheshimu tofauti,
kukuza mazungumzo na ushirikiano kamilifu, kwa ajili ya kumwendeleza kila biandamu
kiroho na kimwili pia ili yaliyokwisha anzishwa tayari, eyaweze kuhakikisha maisha
bora ya baadaye kwa kila mtu, na kwa namna ya kipekee hasa kwa ajili ndugu wake
kwa waume wanaoishi katika mazingira magumu zaidi. Papa alimhakikishia Rais Raffael,
uwajibikaji na ushirikiano wa kanisa katika kmwendeleza mtu kiroho na kimwili pia.
Papa alieleza na kukiri kuianza ziara yake akiwa amejawa na msisimko na matumaini
makubwa kwa siku za usoni, kwa kuweka tumaini lake kwa Wakristo wenye kumtambua
Kristo kama Mwanga unaomulikia maisha yao kama ulivyo mwanga wa jua, na mwanga wa
mwezi kama Kanisa, jamii ya waamini. Alisisitiza hakuna mtu mwingine anayeleta ukombozi
, isipokuwa Yesu Kristo, kwa mwanga wake ambaye ni yeye mwenyewe. Papa alieleza na
kuomba ili kwamba , siku zijazo, ziweze kutufanya sisi sote kuutambua waziwazi mwanga
huu na kuwa karibu nao kama vile jua linavyotuangazia kutoka juu. Na ili kila mmoja
wetu, aweze kupata tafakari za kweli juu ya mwanga wa Kristo na upendo wake.
Tokea hapo Papa alipeleka salaam zake za upendo kwa watu wote wa Ecuador, kutoka
pande zote za msitu ya Amazoni hadi katika visiwa vya Galapagos ,akisema pasiwepo
kamwe mtu asiyetoa shukurani zake kwa Mungu kwa majaliwa yake yote. Na aliwataka
kwamwe wasipoteze uwezo wa kulinda mazuri yote ya nchi yao, hata yale yanayo onekana
kuwa madogo na mepesi, ikiwemo huduma kwa watoto wao na wazee wao, na pia wawe na
matumaini kwa vijana na kuwa daima kuheshimu watu wao na uzuri wa umoja wa nchi yao.
Papa alieleza na kuomba Moyo Mtakatifu wa Yesu na Moyo Safi wa Maria, ujalie kila
neema na baraka kwa taifa la Ecuador.
All the contents on this site are copyrighted ©. |