2015-07-01 12:46:00

Hatua makini zaidi zahitajika kufanikisha afya bora duniani.


UNICEF-WHO:  Duniani kote,  mtu mmoja kati ya watu watatu katika kundi la watu bilioni 2.4 hawana huduma za usafi kiafya - ikiwa ni pamoja na watu 946,000,000 wanaoishi bila kuwa na vyoo.  Shirika la kuhudumia Watoto  UNICEF na shirika la Afya la Dunia,  WHO, wameandika katika Ripoti yao , inayosisitiza ufuatiliaji mpya katika mafanikio ya Usafi na maji safi ya kunywa. Ripoti ya mwaka  2015, inayo toa tathimini ya mwisho, juu ya Mafanikio na mapungufu ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia yanayo maliza muda wake mwaka huu.  

Ripoti hiyo inasema , kukosekana kwa mafanikio katika uwanja wa usafi wa mazingira,  kunaendelea  kuwa kitisho kwa  maisha ya watoto na pia hudhoofisha faida za afya, zinazofanikishwa katika upatikanaji wa maji safi ya kunywa,  WHO na UNICEF zimeonya.

Ripoti imekiri kwamba, upatikanaji wa vyanzo vilivyo boreshwa vya  maji ya kunywa, umekuwa na  mafanikio makubwa kwa nchi na jumuiya ya kimataifa, ambamo  watu wapatao bilioni 2.6 wameweza kuwa na vyanzo vya kuaminika  tangu mwaka 1990. Hii ina maana ya asilimia 91% ya idadi ya watu duniani sasa ina maji ya kunywa.  Katika eneo la Kusini mwa Sahara, kwa mfano, watu 427,000,000 wamewezeshwa kupata maji safi.  Lakini matokeo katika suala la maisha ya mtoto, yanasikitisha kutokana na  leo hii, bado watoto karibia elfu moja wenye umri  chini ya miaka mitano, maisha yao hukatishwa  kila siku kutokana na maradhi ya kuhara  yanayo sababishwa na maji machafu  na usafi duni katika mazingira, ingawa  hali imeboreka ikilinganishwa na miaka 15 iliyopita, ambako watoto zaidi ya watoto 2,000 walipoteza maisha kila siku .

Taarifa inaendelea kubaini kwamba, kwa upande mwingine, maendeleo katika sekta ya afya yameathiriwa na uhaba wa uwekezaji katika kampeni za kubadili tabia, ukosefu wa bidhaa za bei nafuu kwa maskini, na tabia za kijamii, hasa katika kubadili mazoea ya  kujisaidia  ovyo vichakani badala ya kutumia vyoo. Takwimu zinaonyesha dunia imeshindwa kufikia lengo la Maendeleo ya Millenia  lililotaka watuwote duniani kufikia mwaka huu 2015, wajisaidie chooni. Leo hii ni asilimia 68% tu ya idadi ya watu duniani hutumia mifumo ya kutosha ya usafi wa mazingira, kukiwa na upungufu wa  asilimia 9 chini ya lengo la Malengo ya Maendeleo ya Milenia, lililotaka walau kufikia asilimia  77%.

Upatikanaji wa maji salama na usafi wa mazingira ni muhimu katika kuzuia na magonjwa ya kitropiki "(NTDs), ikiwa ni pamoja na trakoma, vimelea vya tumboni na kichocho. NTDs kuathiri zaidi ya watu katika nchi 149, ambamo husababisha pia  upofu, ulemavu wa kudumu na kifo.

Taarifa inaendelea kuonya kwamba,hali ya ukosefu wa usafi katika mazingira na vyanzo bora  vya maji,  vitaendelea kuwa kitisho na hatari kwa  watu wengi kuendelea  kufa kutokana na magonjwa yanayohusiana na maji na mazingira machafu, Maria Neira, Mkurugenzi wa Idara Afya ya Umma, katika Shirika la Afya la Dunia, amesisitiza. Upatikanaji wa maji salama na usafi wa mazingira ni muhimu katika kuzuia na utunzaji maradhi 16 ya kitropiki(NTDs. ambayo huathiri zaidi katika nchi 149.

Aidha inatajwa mazoezi ya kwenda haja kubwa katika maeneo wazi pia inahusishwa na kushamiri kwa hatari kubwa ya matatizo ya ukuaji, ikiwemo utapiamlo sugu - ambao huathiri watoto karibia milioni  161 duniani kote, wenye kuwaacha na ulemavu wa kimwili na utambuzi uharibifu. Kwa faida ya afya, ni muhimu zaidi kuharakisha maendeleo katika usafi wa mazingira, hasa katika maeneo ya vijijini," amesema Neira. Katika maeneo ya vijijini nyumba ya 7 kati ya 10 watu hawana vyoo.Hili ni jambo la hatari kubwa. 

WHO na UNICEF zimeweka  mkazo katika muhimu wa  kujifunza kutoka mipango ya maendeleo ya vipindi vilivyopita, 1990-2015 ili kuhakikisha kuwa malengo mapya  yajaza mapengo ya  kukosekana kwa usawa na kufikia upatikanaji wa maji na usafi wa mazingira kwamba, kwa kufanya hivyo,dunia inahitaj kuwa na takwimu sahihi kwa ajili ya kuweza kubaini idadi na maeneo ambako bado kuna upungufumkubwa ikilinganishwa na wastani wa kitaifa;
.kuwa na ni aza kufanikisha malengo katika maeneo yenye hali ngumu sana kufikia, hasa watu maskini katika maeneo ya vijijini;
.kuwa na ubunifu kiteknolojia na mbinu ya kuleta ufumbuzi endelevu katika usafi wa mazingira kwa jamii maskini kwa bei nafuu;
.kutoa kipaumbele kikubwa katika kuboresha usafi wa ndani ya nyumba, shule na vituo vya afya.

Chanzo :UNICEF/WHO 2015 Report- 

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.