2015-06-22 15:52:00

Askofu mkuu Luis Mariano Montemayor ateuliwa kuwa Balozi mpya wa Vatican, DRC


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Luis Mariano Montemayor, kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Jamhuri ya Watu wa Congo. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Montemayor alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Senegal, Guinea-Bissau, Cape Verde na mwakilishi wa kitume nchini Mauritania.

Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Luis Mariano Montemayor, alizaliwa kunako tarehe 16 Machi 1956 hujo Argentina. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapewa Daraja Takatifu la Upadre hapo tarehe 16 Novemba 1985. Kunako tarehe 19 Juni 2008 akateuliwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu na hatimaye, kuwekwa wakfu hapo tarehe 6 Agosti 2008.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican. 








All the contents on this site are copyrighted ©.