2015-06-13 17:03:00

Tunadhulumiwa na kunyanyaswa, hakikisheni kwamba, hatusahauliki!


Baraza la Maaskofu Katoliki Italia, CEI limechangia kiasi cha Dolla za kimarekani millioni moja na laki mbili kwa ajili ya kuwasaidia Wakristo wanaoendelea kuteseka nchini Iraq. Hivi karibuni, Askofu mkuu Bashar Warda wa Jimbo kuu la Erbil, Iraq aliomba msaada kutoka kwa wasamaria mwema kutoka sehemu mbali mbali za dunia ili kuhuudumia familia 13, 000 za wakimbizi zinazopata hifadhi Jimboni mwake. Kutokana na kuguswa kwa mahangaiko ya Wakristo huko Iraq, Baraza la Maaskofu Katoliki Italia limetoa mchango huu ili kusaidia familia pamoja na kuchimba visima vinne vya maji.

Fedha hii pia itasaidia kuendeleza ujenzi wa shule kwa ajili ya wakimbizi huko Erbil. Shirika la misaada la Kanisa Katoliki Italia, litaendelea kutoa huduma ya chakula kwa familia za wakimbizi na watu wasiokuwa na makazi huko Erdil katika kipindi cha mwezi Agosti, 2015.

Askofu Nunzio Galantino, Katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Italia, CEI anasema kwamba, kuna maneno ambayo yamenata akilini mwake, aliposikia Wakristo huko Iraq wanasema, “tunadhulumiwa na kunyanyaswa, akikisheni kwamba, hatusahauliwi”. Hii ni dhamana ya upendo na mshikamano wa kidugu inayotekelezwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Italia kwa ajili ya wakristo huko Iraq.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.