2015-06-04 15:23:00

Waraka wa Papa Francisko kuhusu mazingira kuzinduliwa 18 Juni 2015


Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kuzindua Waraka wake mpya wa kichungaji kuhusu mazingira, hapo tarehe 18 Juni 2015. Huu ni waraka ambao unatarajiwa kutoa mchango mkubwa katika mchakato wa utunzaji bora wa mazingira kwa kukazia kanuni maadili. Mengi zaidi yatafafanuliwa wakazi wa uzinduzi wa waraka huu ambao unatolewa wakati ambapo Jumuiya ya Kimataifa inajiandaa kufanya mkutano wa kimataifa kuhusu mazingira, mwezi Desemba, 2015 huko Paris, Ufaransa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.