2015-06-04 15:35:00

Rais Vladimir Putin kukutana tena na Papa Francisko 10 Juni 2015


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano, tarehe 10 Juni 2015, majira ya jioni, anatarajiwa kukutana na kuzungumza na Rais Vladimir Putin wa Russia. Itakumbukwa kwamba, hii itakuwa ni mara ya pili kwa Rais Putin kukutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko. Kwa mara ya kwanza anasema Padre Federico Lombardi msemaji mkuu wa Vatican kwamba, viongozi hawa wawili walikutana mjini Vatican kunako tarehe 25 Novemba 2013.

Rais Putin akiwa nchini Italia, anatarajiwa pia kukutana na kuzungumza na Rais Sergio Mattarella wa Italia pamoja na Bwana Matteo Renzi, Waziri mkuu wa Italia. Rais Putin atatembelea Onesho la Chakula Kimataifa, Expo Milano 2015.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.