2015-06-02 09:56:00

Bikira Maria Mama wa Mungu na Kanisa utuombee!


Wanasayansi, wasomi, wanafalsafa, washindi wa tuzo mbali mbali za kimataifa, watu wasioamini na watu wa kawaida, wengi wao wamekuwa na jicho la pekee kabisa kwa Bikira Maria, Mama wa Mungu na Kanisa, kwa kutambua mchango na dhamana yake katika historia ya kazi ya ukombozi. Ni maneno yaliyotolewa na Kardinali Angelo Comastri, Makamu Askofu wa Mji wa Vatican, Jumapili jioni tarehe 31 Mei 2015 wakati wa kufunga rasmi mwezi wa Mei, uliotengwa rasmi na Mama Kanisa kwa ajili ya heshima na ibada kwa Bikira Maria.

Ibada ya Rozari Takatifu, muhtasari wa Injili, ilitanguliwa na maandamano ya waamini waliokuwa wamebeba mishumaa mikononi mwao, hadi kwenye Madhabahu ya Biki ra Maria wa Lourdes, yaliyoko kwenye bustani za mji wa Vatican. Watawa wa mashirika mbali mbali ya kitawa na kazi za kitume wameshiriki kwa ukamilifu bila kuwasahau viongozi mbali mbali mbali wa Kanisa kutoka ndani na nje ya Vatican wameshiriki pia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.