2015-05-29 15:06:00

Slovenia na Vatican kuendeleza mchakato wa upatanisho wa kitaifa


Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 29 Mei 2015 amekutana na kuzungumza na Bwana Miro Cerar, Waziri mkuu wa Slovenia ambaye baadaye amekutana pia na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu  wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Katika mazungumzo ya viongozi hawa, wameonesha kuridhishwa na mahusiano yaliyopo kati ya Slovenia na Vatican. Kwa pamoja wamenuia kuendeleza majadiliano kuhusiana na masuala muhimu kati ya Kanisa na Serikali mintarafu mchakato wa upatanisho wa kitaifa; tunu msingi za maisha ya kiutu na kidini pamoja na kuendelea kushirikiana kwa ajili ya mafao ya wengi. Maskini wanapaswa kupewa kipaumbele cha kwanza.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C. PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.