2015-05-28 15:40:00

Kinzani za kijamii, kisiasa na kiuchumi ni kati ya changamoto kubwa Croatia


Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 28 Mei 2015 amekutana na kuzungumza na Rais Kolinda Grab-Kitarovic wa Jamhuri ya Watu wa Croatia, ambaye baadaye amekutana pia na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameandamana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, katibu mkuu  wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Katika mazungumzo kati ya Baba Mtakatifu na mgeni wake, wamepongeza mahusiano mazuri yalipo kati ya nchi hizi mbili, changamoto ya kuendelea kuimarisha mahusiano haya kadiri ya mikataba iliyoridhiwa na nchi hizi. Viongozi hawa wamejadili kwa kina na mapana kuhusiana na mahusiano kati ya Kanisa na Serikali, kwa ajili ya mafao ya wengi hususan kwa ajili ya kuwategemeza familia na vijana. Baadaye wamegusia pia masuala ya kimataifa na kikanda mintarafu kinzani za kiuchumi, kijamii na kisiasa na changamoto zilizopo kwa sasa kati ya wananchi wa Croatia huko Bosnia na Erzegovina.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.