2015-05-21 16:17:00

Mama Rudo Mabel Chitiga awasilisha hati zake za utambulisho mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 21 Mei 2015 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mama Rudo Mabel Chitiga Balozi mpya wa Zimbabwe mjini Vatican. Balozi Chitiga alizaliwa kunako tarehe 23 Septemba 1960. Alipata elimu yake nchini Zimbabwe na kwenye Chuo kikuu cha Ford Hare na kuhitimu kunako mwaka 1997. Katika maisha yake amewahi kuwa ni mfanyakazi katika Wizara ya maendeleo ya jamii na wanawake Zimbabwe kati ya mwaka 1982 hadi mwaka 1986.

Aliwahi kuteuliwa kuwa Katibu mkuu msaidizi kwenye Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Waziri wa maendeleo ya jamii na wanawake kati ya mwaka 1986 hadi mwaka 1988. Mkurugenzi mkuu wa IRED, Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika kati ya mwaka 1988 hadi mwaka 1996: Mkurugenzi mkuu wa IRED Mikakati ya kimataifa ya IRED kati ya mwaka 1996 hadi mwaka 1997.

Kati ya mwaka 1998 hadi mwaka 1999 alichaguliwa kuwa Katibu mkuu wa IRED na mwakilishi wa Zimbabwe kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa zenye makao yake makuu geneva, Uswiss. Kunako mwaka 2000 hadi mwaka 2006 alikuwa ni Mkurugenzi msaidizi wa Mfuko wa Jumuiya ya Madola. Baada ya mwaka 2008 alikuwa ni mshauri wa kujitegemea hadi kuteuliwa kwake na Serikali ya Zimbabwe kuwa ni Balozi mpya wa Zimbabwe mjini Vatican.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.