Baba Mtakatifu Francisko amekemea jumuiya ya Kikrito kuwa na woga na hofu katika kuiishi imani yake kwa Kristo akisema , Jumuiya hiyo yenye woga na isiyokuwa na furaha, inayoumwa na si jumuiya ya Kikristo, Papa alieleza katika mahubiri yake ya Mapema Ijumaa hii wakati akiongoza Ibada ya Misa katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta Vatican.
Homilia ya Papa ilitafakari maneno makuu mawili :"Hofu" na "Furaha", yaliyokuwa katika liturujia ya siku. Papa ameitaja tabia ya kuwa na hofu kwamba huongoza katika kutenda maovu.Huleta udhaifu na humrudisha muumini nyuma, na hata hupoozesha juhudi zote zake katika imani. Mtu mwenye hofu, hawezi fanya chochote kwa kuwa hajui la kufanya na hivyo humwongoza katika utendaji wenye ubinafsi na matokeo yake ni kutia ngiza kila jambo. Mkristo mwoga ni mtu ambaye bado hajaelewa ujumbe wa Yesu.
Kwa ajili hii Yesu alimwambia Paulo, 'Usiogope’, kwa kuwa tabia ya woga si tabia
ya Kikristo. Kwa maneno mengine Papa anasema, woga ni kuwa na roho aliyefungwa ,
Roho isiyokuwa huru, uhuru wa kutazama maendeleo ya mbele au kutenda mema . Na
hii ni hatari na tabia mbaya. Kwa Mkristo. Papa ameeleza na kuhoji kwa nini Mkristo
awe na woga wakati kuna silaha ya neema ya ujasiri kutoka kwa Roho Mtakatifu , mwenye
kuwapatia Wakristo ujasiri ?
Maelezo ya Papa juu ya woga au hofu pia yaliweka bayana tofauti iliyopo katika kuongopa
ukuu na utakatifu wa Mungu, na woga wa kuogopa kumtaja Mungu mbele ya watu. Tofauti
iliyopo kati ya woga wa kuwa mbele ya Bwana katika kuabudu na woga uadilifu wa Mungu,
na woga wa kumwogopa binadamu mwingine katika kueleza hisia za imani toka ndani ya
moyo. Papa alifafanua, kumwogopa Mungu, hakudhoofishi, wala kuipoozesha imani, lakini
hutusaidia kusonga mbele na utume unaotolewa na Kristo katika neno lake, na hakuna
mtu atakayeiondoa furaha hiyo kwa muumini, kama Yesu alivyosema wakati wa saa ya
maumivu na mateso, kinakuwa ni kipindi cha furaha na amani. Furaha hiyo hugeukuwa
kuwa amani. Na hivyo Mkristo anayeishi katika huzuni na woga daima huyo si Mkristo.
Papa aliendelea kuitafakari furaha ya Mkristo, akieleza kwamba, si furaha nyepesi
ya kufuraha mambo ya kidunia,na wala siyo furaha ya mpito wa muda mfupi, bali ni
furaha ya kudumu inayotoka kwa Kikristo kama zawadi, zawadi ya Roho Mtakatifu. Ni
daima kuwa na moyo wa furaha kwa sababu Bwana ameshinda, Bwana ni Mfalme, Bwana ni
pamoja na Baba, Bwana ndiye anayenitazama na ndiye aliyenituma na kunipa neema yake
na mimi kama mtoto wa Baba ... Na ninafurahia kuwa Mkristo. Mkristo huishi kwa furaha.
"
Papa alieleza na kuzitazama kwa makini jumuiya inayoishi bila furaha akiitaja jumuiya
kamahiyo inamatatizo,inaumwa, imesongwa na maradhi,kwa kuwa imejenga msingi wake
katika mambo ya kidunia . Na ndivyo ilivyo kwa Kanisa lenye woga ,kanisa hilo lina
matatizo ,ndani mwake halina Roho Mtakatifu, Ni Kanisa gonjwa, waamini wake ni wagonjwa
na jumuiya hiyo ina maradhi ya kiroho" Papa inamalizika na sala akimwomba Bwana ,
ashushe roho yake ili sote tuweze kuinuliwe na kuelekea alikoketi Kristo,katika mkono
wa Kulia wa Baba , ainue roho zetu na kuondoa kila jambo lenye kututia hofu na woga
badala yake atupatie furaha na amani yake milele..
All the contents on this site are copyrighted ©. |