Askofu Giampietro Dal Toso , Katibu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya utoaji wa misaada ya Jimbo la Papa kwa wahitaji, Baraza linalojulikana kwa jina "Cor Unum” akishiriki katika Mkutano Mkuu wa XX wa Taasisi ya Kimataifa ya Misaada Katoliki, ” Caritas Internationalis”, ameshukuru uwepo wa taasisi hiyo kimataifa, yenye kuvuviwa na upendo wa kiinjili katika juhudi zake za utetezi wa haki na ustawi wa wote. pamoja na hilo, amesisitiza umuhimu wa kutunza utambulisho na kanuni zinazoongoza Caritas mahali popote duniani.
Askofu Toso, kwa namna ya pekee ametaja umuhimu wa dhana ya ushirikiano, kama chimbuko la nguvu zote za utendaji wa Caritas , kati ya ngazi ya Kimataifa na matawi yake yote ya pembezoni. Alisema , kwa kweli, dhana ya ushirikiano ndani ya Caritas, umethibitisha ukweli kwamba, inawezekana kuwa na vyombo mbalimbali vya kujitegemea, kutenda majukumu yake ya kawaida kwa kushirikiana na wengine. Na ushirikiano huo, hauna maana ya kuondoa uhuru wa kila mmoja . Hivyo, unakuwa si mfumo unaofungwa na uwepo wa serikali moja kuu, lakini ni kinyume chake , kila Ofisi yake kijimbo, na kitaifa hufanya azi zake kwa kujitegemea lakini katika utendaji wenye mshikamano wa pamoja na nchi zingine, katika kukabiliana matatizo yanayofanana.. Kanuni hii , ndiyo nguzo muhimu ya kuuelewa muundo wa Shirika la kimataifa la Caritas Internationalis na wanachama wake kitaifa.
Mons. Tosso aliendelea kuzitazama hali halisi za nyakati hizi na kushukuru kwamba, kuna ushirikiano thabiti kati ya Caritas Intenationalis na huduma za Caritas katika Majimbo, utendaji unaoonyesha uimara wa chombo hiki katika utumishi wa upendo wa Kanisa katika ngazi ya kimataifa na kitaifa , ikiheshimiwa kama shirika la Kidini. Na hatua zilizochukuliwa kuuunda muundo wake mpya wa kisheria, hutangaza wazi kwamba, utendaji wa usharika huu, iwe ndani ya Kanisa au kwa ajili ya dunia, ni lazima kushiriki katika utume wa Kanisa. Kwa kuwa ni upendo katika ukweli, uliojikita katika asili ya Upendo wa Mungu na uzoefu wa Kanisa la Mwanzo, kuuweka upendo katika mazingira yake ya awali, ya kutangaza Neno la Mungu na maadhimisho ya sakramenti, kama kipaumbele cha kwanza sahihi na muhimu kwa Kanisa. Hivyo basi, kabla ya kuigia katika utendaji ngazi za jamii, ni lazima kuthibitisha kwamba hisani za Kanisa, zinakuwa na tabia ya Kikanisa.
Kanuni hiyo, inakuwa ni rejea msingi , katika uanzishaji wa huduma zote za hisani za Kanisa Katoliki na utendaji wake wote, unaelekezwa kwa Mungu, kwa kuhamasishwa upendo kwa jirani, kupia fadhila na utoaji wa msaada kwa kila binadamu, kama Bwana alivyofundisha na kutenda . Ni wazi, na ni muhimu kwa Wakristo , kutafakari na kutafuta ufumbuzi wa pamoja kwa matatizo mengi ya umaskini na kutengwa kama sharti la haki. Lakini, wakati huohuo ni muhimu pia kufikiria uwepo wa mbinu zinazoweza fanikisha ufanisi wa huduma hii ya kanisa, bila kuhatarisha au kupoteza tabia yake ya Kikristo katika kazi zake. Zaidi ya yote, jinsi kanisa linavyoweza kukabiliana na mateso ya binadamu na umaskini, kupitia huduma ya huruma na wema unaofundishwa katika moyo wa ujumbe wa injili.
Hilo huhakikisha utimizaji wa wajibu msingi na muhimu ndani ya Kanisa na jamii kwa ujumla. Hivyo isisahaulike kwamba, Caritas ina utambulisho tofauti na taasisi na vyama vingine vingi. Katika Kanuni zake, Caritas katika ngazi ya jimbo, ni chombo cha Askofu kwa ajili huduma katika utume wa upendo na mshikamano wa Askofu kwa watu wahitaji. Utambulisho huo ndiyo hasa hutofautisha Caritas na taasisi au vyama vingine vinavyoweza anzishwa na waamini Katoliki Lengo la kwanza la Caritas ni kuhamasisha watu juu ya upendo na utume wa Kanisa, ili watu waweze kuona upendo na huruma ya Mungu. N Caritas inaweza kutoa mchango muhimu kufikia lengo hili, kama Papa Francis, alivyoomba, Caritas kuwa chombo Kikuu cha Kanisa Katoliki katika utoaji wa huduma za hisani za Kanisa,katika kuwaleta watu karibu zaidi na Mungu na ili Kanisa lenyewe liwe mlango wa upendo na wema.
All the contents on this site are copyrighted ©. |