2015-05-09 12:44:00

G7: Madambiu ya mkutano wa Vijana erlin


Alhamisi wiki hii mjini Berlin Ujerumani, Shirika la Kuhudumia Watoto Unicef na mbia wake Wizara ya ustawi wa jamii na familia, Wazee , wanawake na vijana Ujerumani,  walianza Mkutano wa Kimataifa wa Vijana unaojulikana kama  G7 wa Vijana  unaohudhuriwa na Vijana 54 kutoka nchi 19. Mkutano huu wa vijana wa G7 unajadili masuala muhimu yanayowahusu na kwa lengo la kutaka kuyawasilisha kama sauti ya vijana katika mikutano wa kimataifa. 

Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF nchini Ujerumani , Christian Schneider , akiuzungumzia mkutano huu amesisitiza kwamba, watoto na vijana wana haki ya kutoa maoni yao na kusikilizwa katika masuala yote yanayowahusu. Vijana pia wanatakiwa kuwajibika katika utendaji wa maisha ya kijamii ya  kila siku. Na hivyo wana haki ya kupewa fursa ya kutoa maoni yao.

Wakiongozwa na  kauli mbiu "wajibu na utendaji ", wajumbe wa mkutano huu kutoka nchi 19, watakuwa pamoja kwa muda wa karibia wiki nzima   mjini Berlin Mei 07-13 kujadili ajenda ya G7, kama maandalizi ya mkutano mwingine utakaofanyika Elmau, Bavaria , mwezi ujao 07-08 Juni . Jumatatu ijayo, wajumbe wa mkutano unaoendelea watakuta  Kansela Angela Merkel wa Shirikisho la Ujerumani na Waziri Manuela Schwesig, Waziri wa masuala ya vijana Ujerumani na kwa pamoja watajadili matokeo ya utafiti wa G7 kama  mfano wa  kioo wa mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa G-7 nchi, ambazo ni  Ujerumani, Ufaransa, Uingereza, Canada, Italia, Japan na Marekani. Wajumbe vijana kutoka nchi hizi , ni mjini Berlin pamoja na  wenzao kutoka nchi kadhaa za  EU na Afrika,  Finland, Ugiriki, Ireland, Poland, Ureno na Slovenia. Ethiopia, Jamhuri ya Dominika, Liberia, Zambia, Senegal na Afrika Kusini watashiriki katika mijadala.

Wajumbe vijana wanajadili  taarifa juu ya masuala yafuatayo ya G7:
• "Linda dunia yetu": kulinda mazingira, hasa mazingira ya bahari, kwa kutumia kwa ufanisi rasilimali na mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.
• "Kujenga afya bora kwa wote kwa maisha ya baadaye,  kama kupitishwa kwa maisha ya afya bora na mapambano dhidi ya magonjwa - hasa yenye  kuathiri maskini - na usugu wa vijidudu katika matumizi ya dawa za  antibiotiki.
• "Uwezeshaji wa Wanawake: kujenga usawa baadaye kwa ajili ya wote": wenye lengo la upatikanaji wa elimu na uundwaji wa haki sawa kwa wanawake na wanaume, wasichana na wavulana.
• "Haki Uchumi" ambayo ni masuala ya kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kutafuta viwango sawia kwa ajili ya kuwa na minyororo wa ugavi wa haki na kupambana na umaskini.








All the contents on this site are copyrighted ©.