2015-05-04 14:45:00

Kitovu cha kimataifa kuwaunganisha wafugaji chaanzishwa


Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na wabia wengine,limezindua mtandao mpya wa kupeana habari utakaotumiwa na Mamilioni ya wafugaji duniani kote, tangu wafungaji  Wabedui wa Afrika Kaskazini  hadi  huko Sherpa Nepal na Navajo  Amerika ya Kaskazini,ambamo wataweza kupeana ujuzi mpya kupitia njia ya mtandao. Mtandao huo  hasa unelengo la kuinua sauti za wafungaji katika mijadala ya sera za kimataifa  na upatikanaji wa  habari muhimu kwa ajili ya  kuimarisha maisha ya wafungaji..

Mtandao huo ulizinduliwa na Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) na washirika wake, kama kitovu cha maarifa kwa Wafugaji, kitakacho wezesha  wafugaji kupeana habari kupitia simu za mkono, kukutana na kujadili masuala  yanayowahusu katika ubunifu wa ufugaji na  kilimo au sheria za ardhi na kupata ufumbuzi wa pamoja katika changamoto za kawaida zinazo wakabili.

Kifaa hiki cha Online, pia kitawezesha upatikanaji wa taarifa na takwimu za wafungaji kwa haraka zaidi kwa ajili ya tafiti na mawasiliano juu ya ufugaji kwa dunia nzima ya wawakilishi wafugaji, na kama ukumbi wa majadiliano ya wafugaji na taasisi shiriki. Na hivyo unalenga kuziba pengo la  kutotambuliwa na dunia kwa  kipindi cha kirefu, hasa ukosefu wa majadiliano maalum juu ya wafugaji katika  sera za kimataifa, na haja makini  ya kuwaunganisha pamoja katika kutoa majawabu kwa  changamoto zinazokabili jamii za wafugaji.
 

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa FAO, Helena Semedo , ameutaja mtandao huu kwamba ni  muhimu kwa kundi hili la kijamii, ambao huwa na  uwezo wa kuzalisha chakula, hata mahali  ambapo hakuna uwezekano wa mazao, kupandwa. Na hivyo inakuwa nyenzo ya kufanikisha  madai yao kusikilizwa na jumuiya ya kimataifa.  Ni mtandao unaunganisha  jamii maalumu za wafugaji ,  Mabedui wa  Afrika Kaskazini na Rais ya Uarabuni, Wamasai wa Afrika Mashariki, Wanavajo wa Amerika ya Kaskazini, Washerpa wa Nepal, na Wasami wa Scandinavia, kama wazalishaji wakuu wa mifugo wanaotupatia  nyama, maziwa, ngozi  na  manyoya, na katika nchi nyingi huongeza zaidi  nusu ya pato la taifa (GDP).

Juhudi hizi mpya pia huunganisha wafugaji na taasissi za kimataifa kama umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya na mashirika ya (IFAD), Umoja wa Kimataifa wa Hifadhi ya Asili (IUCN), Umoja wa Mataifa Mpango wa Mazingira (UNEP), Benki ya Dunia na mashirika yasiyo ya kiserikali , ikiwa ni pamoja na mashirika na vyama vya wafugaji vya kiraia.








All the contents on this site are copyrighted ©.