2015-04-30 15:23:00

Tanzia: Kardinali John Canestri amefariki dunia


Mama Kanisa anasikitika kutangaza kifo cha Kardinali Giovanni Canestri, kilichotokea siku ya Jumatano. Baba Mtakatifu mara baada ya kupata taarifa hizi amepeleka salaam zake za rambirambi kwa Kardinali Agostino Vallini, Vika wa Jimbo la Roma akionyesha masikitiko yake kwa kifo cha mtumishi huyu wa Mungu, aliyemtaja kwamba, amelitumikia Kanisa kwa moyo wa dhati, akiwa amejawa na imani na unyenyekevu mkuu, katika huduma yake ya muda mrefu kama Padre na pia kama Askofu, akiihudumia  Injili na roho za waamini aliokabidhiwa na Bwana.

Papa amekumbuka fadhila na ujasiri wa marehemu  katika kazi zake, hasa wakati akiwa Makamu wa Paroko , wakati wa miaka migumu ya vita , katika vitongoji  maskini vya nje  kidogo katika Roma , ambavyo vilikabiliwa na hali ya ngumu ya  mateso na umasikini . Na pia wakati akiwa  Paroko wa vijiji viwili , ambako kwa namna ya kipekee aliweka mkazo zaidi katika  nia  za  kuwaelimisha vijana hasa katika kuiona ya furaha ya imani.

Na baadaye aliteuliwa kuwa msaidizi Askofu wa Roma, kazi aliyoifanya kwa majitolea makubwa katika mtazamo wa kichungaji na kihali pia kwa watu aliokuwa akiwaongoza, na pia alishiriki katika kazi ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican. Papa Francisko amaetia nguvu Vika wa Roma akisema,wako pamoja katika sala za kuiombea roho ya Marahemu Kardinali Canesrti ,na ametoa Baraka zake za Kitume ka wote wanaoombeleza msiba huu. 

Aidha taarifa zaidi zimetolewa kwamba, kwa ajili ya msiba huu, Jumamosi, Mei 2, 2015, saa 8:30 asubuhi, katika Madhabahu  Kuu ya Kanisa Kuu  la Mtakatifu Petro, kutafanyika Ibada ya mazishi, itakayoongozwa na Kardinali Angelo Sodano , Dekano wa Dekania ya Chuo cha  Makardinali. Maziko ya Marehemu Kardinali Giovanni Canestri, Askofu wa Jina wa  Kanisa Kuu la Mtakatifu  Andrea della Valle, na Askofu Mkuu Mstaafu  Genoa.
Mwisho wa Liturujia Mazishi,  Baba Mtakatifu ataongoza sala ya mwisho, kumwombea Marehemu pumziko la amani. 

Kardinali Canestri , alizaliwa Septemba 30, 1918, kaiak jimbola Castelspina , jimboni Alexandria . Alipadrishwa mjini Roma Aprili 1941, katika Kanisa Kuuu laYohane wa Lateran, ambako alihudumia kama Mkurugenzi katika Idara ya mambo ya Kiroho katika Seminari Kuu ya Jimbo la Roma.  Na aliteuliwa kuwa Askofu na Papa Yohane XXIII,kama Askofu Msaidizi wa Vika wa Roma . Na laishiriki katika Mkutano Mkuu wa Pili wa Vatican, ambamo alitoa mchango wake katika mada nyingi zinazohusiana na uekumeni na uhuru wa kidini.

Na mwaka 1971, akiwa Askofu aliteuliwa  kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Papa huko Tortona,na  miaka minne baadaye alifanywa kuwa Mkuu wa Kanisa la Tortona , na baadaye Papa Paulo VI, alimrudisha Roma kama Msaidizi wa Vika wa Jimbo la Roma.Na mwaka 1984, Papa Yohane Paulo II,alimteua kuwa Askofu Mkuu wa Cagliari , na baada ya miaka mitatu , akateuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Genoa Bobbio,akichukua nafasi ya Kardinali Giuseppe Siri.

Askofu Mkuu Canestri alifanywa kuwa Kardinali na Papa Yohana Paulo II, mwaka 1988. Na aliendelea kuwa Askofu Mkuu wa Genoa hadi alipostaafu mwaka 1995.

Kwa kifo chake , Baraza la Makardinali sasa limebaki na wajumbe 222 ambao kati yao walio  chini ya miaka 80 wenye haki ya kupiga kura katika kikao cha Conclave ni 120 . 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.