2015-04-30 11:54:00

Mageuzi Vatican: Papa aunda Tume ya Vyombo vya Mawasiliano vya Vatican


Baba Mtakatifu Francisko kwa kuzingatia ushauri uliotolewa na Baraza la Makardinali washauri kuhusu marekebisho makubwa yanayopaswa kufanyiwa kazi kwenye Sekretarieti ya Vatican, kama sehemu ya utekelezaji wa maamuzi yaliyofanywa na Makardinali wakati wa vikao vyao elekezi, ameamua kuunda Tume ya Vyombo vya Mawasiliano vya Vatican, V.M.C itakayokuwa chini ya Monsinyo Dario Edoardo Viganò. Mkurugenzi mkuu wa Kituo cha Televisheni cha Vatican, CTV.

Wajumbe wa Tume hii ni pamoja na:

Dr. Paolo Nusiner, Mkurugenzi mkuu wa Avvenire

Mons. Lucio Adrian Ruiz, Mkuu wa kitengo cha mitandao na mawasiliano Vatican

Padre Antonio Spadaro, Mkurugenzi wa Jarida la “La Civiltà Cattolica” pamoja na

Mons. Paul Tighe, Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Jamii.

Tume ya Vyombo vya Mawasiliano vya Vatican itakuwa na dhamana ya kupembua kwa kina na mapana mapendekezo yaliyotolewa na Baraza la Makardinali washauri katika kikao chao cha tarehe 23 Aprili 2015.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.