2015-04-28 09:43:00

Papa ahimiza mwendelezo wa majadiliano kati ya dini nchini Benin


Baba Mtakatifu Francisko mapema Jumatatu  27 Aprili 2015, ,  akihutubia kikundi cha  Maaskofu kutoka Benin Afrika Magharibi , alishukuru kwa  huduma yao, yenye kuushuhudia upendo wa Kristo kupitia utendaji wamiradi mbalimbali ya  Kanisa, nchini Benin. Na hivyo akawahimiza waendelee kutoa msaada katika maisha ya kiparokia, kuhamasisha idadi kubwa ya waamini kushiriki katika maadhimisho ya kanisa kwa moyo wa dhati na kufanya mabadiliko ya kiroho hasa kwa ajili ya miito na ukuzaji wa majadiliano kati ya dini .  Maaskofu hao wako Roma kwa ajili ya ziara ya kitume ya ad limina Viist, wakiongozwa na  Askofu Antoine Ganyè , Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Benin.

Baba Mtakatifu alionyesha pia kutambua changamoto halisi  mfululizo wanazokabiliana nazo Maaskofu  na hasa matatizo makubwa yanayohusiana na masuala ya kifamilia. Alionyesha tumaini lake kwamba, Sinodi ya Pili juu ya Familia itakayofanyika Roma Mwezi Oktoba , itaweza jaribu kupata  baadhi ya majawabu. Na hivyo aliwahimiza waendelee bila kuchoka  na jitihada za kusaidia familia, katika yote mawili  kiroho na katika maisha ya kila siku. Papa alionyesha kutambua kwamba  ndoa ni moja ya wito mgumu katika maisha, kutokana na hali halisi za  kijamii na kiutamaduni.  Na hivyo inakuwa ni hitaji la lazima kwa viongozi wa Kanisa, kusaidia kuunda familia za kweli zilizosimikwa katika misingi ya upendo wa kudumu, kwa kuwa familia daima ni ukweli, unaotakiwa na Mungu. Ndoa ni zawadi kutoka  Mungu mwenyewe ambayo huwaletea watu na jamii kwa ujumla furaha amani na utulivu. Familia Papa alisema ni kitengo msingi cha  jamii.

Aidha Papa alizungumzia changamoto nyingine inayowakabili  Maaskofu wa Benin, kuwa ni matatizo ya vijana na elimu, na hapohapo akatoa shukurani zake kwa juhudi zinazofanywa na Kanisa nchini Benin ambako wameweza kufungua shule Katoliki nyingi katika majimbo yao. Na hivyo akazungumzia umuhimu wa kukutana katika mazungumzo na tamaduni mbalimbali za kidini, hasa na  Uislamu. Na alishukuru kwa Benin , kuwa mfano bora wa maridhiano kati ya dini , lakini pia akaonya  kwa ajili ya kulinda urithi huo teke, umuhimu wa kuwa macho kutokana na hali za kisasa za mwingiliano wa watu kimataifa.

Na hivyo, kupitia ukuzaji wa maelewano na haki katika Makanisa ya mahalia majimboni mwao,  unakuwa ni wajibu  kwa Maaskofu, kuwa watendaji wakuu wa maendeleo katika nchi yao.  Pia Papa alikitazama kipeo cha uchumi wa dunia kinachoathiri mataifa mengi , akisema ni muhimu kutenda kinyume na wimbi la sasa , kuwa kinyume na utamaduni wa ulaji , utamaduni wa kufuja mali ulioenea kila mahali kama ilivyoelezwa katika waraka wa Injili ya Furaha (cf. Evangelii Gaudium, 53) na kusambaza maadili ya Injili ya ukarimu na kukutana.

Papa aliendelea kuwakumbusha  Maaskofu kwamba, huduma ya upendo ni utume wa Kanisa, wenye kuunyesha asili yake , na hivyo alitoa mwaliko kwa watawa wote kuliishi hilo kwa mkazo zaidi hasa katika mwaka huu wa maadhimisho ya Maisha yaliyowekwa wakfu , akionyesha pia kutambua majitolea  ya ukarimu wa makuhani katika utumishi wa Injili.

Kwa namna hiyo alitoa maoni pia juu ya wingi wa  miito ya Upadre Benin, kwa kuwataka  Maaskofu,  kuwa na upendo wa kibaba  kwa mapadre wao, na hasa  kukuza ushirikiano na udugu, ndani ya  familia ya kikuhani na kutunza wale wanaohitaji,  na  kwa moyo wa  ukarimu kugawana utajiri wa rasilimali na makanisa mengine yenye kupungukiwa.Na mwisho alihitimisha kwa kuonyesha kutambua mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Kanisa na mamlaka za kiserikali . Na kwa sauti ya Kanisa kusikilizwa na kupendwa. Na hivyo Papa aliwalika wote waendelee kushiriki katika maisha ya umma katika taifa lao na ujenzi wa mahusiano bora zaidi kati ya makundi mbalimbali ya kijamii.








All the contents on this site are copyrighted ©.