2015-04-25 09:15:00

Mons. Piergiorgio Bertoldi ateuliwa kuwa Balozi mpya wa Vatican B.Faso


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Piergiorgio Bertoldi, kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Burkina Faso na Niger na kumpandisha hadhi kuwa ni Askofu mkuu. Askofu mkuu mteule Bertoldi alizaliwa huko Varese, Jimbo kuu la Milano, hapo tarehe 26 Julai 1963. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikuhani, akapewa Daraja Takatifu la Upadre tarehe 11 Juni 1988. Amejiendeleza na hatimaye akapata Shahada ya uzamivu katika Sheria za Kanisa .

Tarehe Mosi, Julai 1995 akaanza utume wa kidiplomasia na amewahi kutekeleza dhamana hii kwa mara ya kwanza kwenye Ubalozi wa Vatican nchini Uganda, Jamhuri ya Congo, Colombia, Yugoslavia ya zamani, Romania, Iran na Brazil.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.