2015-04-23 09:54:00

Papa kutembelea Cuba, akiwa njiani kuelekea Marekani, Sept. 2015


Baba Mtakatifu Francisko amekubali mwaliko kutoka kwa viongozi wa Serikali ya Cuba pamoja na Baraza la Maaskofu Katoliki Cuba wa kufanya hija ya kitume nchini Cuba wakati atakapotembelea Marekani, mwezi Septemba 2015. Hayo yamebainishwa na Padre Federico Lombardi Msemaji mkuu wa Vatican, Siku ya Jumatano tarehe 22 Aprili 2015, wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari mjini Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko akiwa Jimbo kuu la Washington, DC, hapo tarehe 23 Septemba 2015 anatarajiwa kumtangaza Mtawa Junipero Serra,Mtume wa calfonia, aliyeonesha ushuhuda wa imani yake kwa Kristo na Kanisa lake, akawatangazia Habari Njema ya Wokovu Watu wa Mungu wanaoishi mjini Calfonia. HIja hii ya kitume, itamwezesha Baba Mtakatifu Francisko kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya Siku ya Familia Kimataifa, itakayoadhimishwa Jimbo kuu la Philadelphia. Baba Mtakatifu atatembelea na kuzungumza na wanachama wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa sanjari na kuhutubia katika Senate ya Marekani, tukio la kihistoria.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican. 








All the contents on this site are copyrighted ©.