2015-04-22 11:08:00

Italia yasema -Changamoto ya uhamiaji yahitaji mkakati mbinu mpya.


Waziri Mkuu wa Italia, Mateo Renzi , mapema Jumatano akizungumzia changamoto ya wahamiaji Ulaya, kabla ya kushiriki katika kikao cha Bunge la Ulaya kinachofanyika kesho Alhamisi,  alitumaini Bunge la Ulaya litafanya majadiliano ya kina , yenye kutambua haja ya  kutengeneza mkakati mbinu mpana zaidi wa kudumu , katika kukabiliana na wimbi la wahamiaji na wakimbizi ,badala ya kuwa na majibu ya mpito ya kurashia rashia harakaharaka, kama kuharibu vyombo vinavyotumika kusafirisha wahamiaji  kinyume cha sheria.

Waziri Mkuu Renzi , alieleza hili akiwa  katika ukumbi wa  Bunge  la Italia  Montecitorio,  ambamo alitaja umuhimu  wa  Wabunge  kufikiria kwa kina zaidi, sababu msingi zinazozua wimbi hili jipya kubwa la uhamaji kwa  nyakati hizi , kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma. Alisema hasa ni kujali nini kinaendelea Afrika.   Bila kuanzia huko , majibu mengine yatakuwa ni majibu ya mpito ambayo hayatasaidia kusitisha  ukatili unaoendelea kuangamiza  maisha ya wana wa Afrika kwa wingi,   wanaovuka bahari ya mediterrannea.  Alieleza hili katika mtazamo  makini kwamba, wakimbizi wanaopoteza maisha si tu kutoka Libya au Syria lakini kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika hasa ambako kuna matatizo ya njaa, vita na mgawanyiko wa  Mabwana wa kisiasa.

Kwa hiyo akasema, mbele ya sura hii ya  uhamiaji  kutoka Afrika, Bunge la Italia , kama inavyotakiwa pia kwa Bunge la Ulaya, wanawajibu wa kutengeneza mpango  thabiti wa miakamingi  ijayo, kwa  Italia na jukumu lake kama daraja la  Ulaya na
Afrika.  Na ametoa wito kwa  mamlaka zote ya kisiasa, kutogawanyika  katika utoaji wa jibu thabiti linalofaa katika kukabiliana na changamoto hii.  Na kwamba ni lazima kutazama kwa makini asili ya kuenea kwa utamaduni wa ugaidi, kama wanataka kushinda vita vinavyo  angamiza wazo la dunia juu ya nguvukazi watu na juu ya  utamaduni.  Hivyo jibu la kiufundi, kama ni nini kinazamisha boti, haliwezi kutatua mgogogro huu, bali hasa ni kutatufa kwa nini  watu wanahama katika nchi zao. Bunge la Jamhuri  ya Italia lina wajibu wa kutoa jibu lake katika hili.

Wakati huohuo , Mtandao wa Radio3 Mondo , umeandika, Mtandao wa uhalifu wa Italia maarufu kwa jina la  Mafia, umebadilisha maeneo yake ya kazi kwa kuhamia Afrika , kama eneo lake  jipya  kwa shughuli zake.  Leo hii Afrika,inathaminiwa sana na wapenda magendo nautajiri wa harakaharaka kutokana na   utajiri wa maliasili zake. Afrika imekuwa ni siri msingi  wa utendaji wa Mafia. Afrika  kama chanzo kikuu cha  migodi ya almasi, dhahabu, vilabu vya usiku na maeneo makubwa ya aridhi wanayojipatia kwa urahisi na uwezekano wa kumiliki miradi mingi kwa njia za rushwa na magendo. .  

Radio3 Mondo, inasema , watu wenye mapenzi mema na Afrika ni muhimu kujiuliza ni njia zipi zinatumiwa na mfumo huo uliofichama wa Mafia kunufaika na utajiri wa Afrika ? Na  iwapo  jumuiya ya  kimataifa  kweli inafuatilia kwa nia makini kukomesha kuenea kwa  mipango ya uchumi angamizi  na matokeo yake mabovu kwa jamii Afrika. Redio hiyo imenukuu Chama cha Waandishi a Habari Vijana   IIRPI, kwa kushirikiana na Mtandao wa Afrika wa Vituo kwa ajili ya Upelelezi  ANCIR, ambao wameandika kwamba,  Uchunguzi wa kimataifa unaoonyesha mtandao wa utendaji wa mafia kwa undani, umeingia katika mataifa  13 ya nchi za Afrika.  








All the contents on this site are copyrighted ©.