2015-04-21 14:54:00

Sr. Stefani Teiefenbacher, C.P.S. ameuwawa kikatili Afrika ya Kusini


Baba Mtakatifu Francisko anasema, bado kuna damu ya Wakristo inayoendelea kumwagika sehemu mbali mbali za dunia. Sista Stefani Teiefenbacher mwenye umri wa miaka 86 wa Shirika la Masista wa Damu Takatifu ya Yesu, (CPS) aliyekuwa anafanya utume wake nchini Afrika ya Kusini, ameuwawa kikatili usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita huko Kwazulu Natali.

Taarifa zinabainisha kwamba, Marehemu Sr. Teiefenbacher, Jumapili asubuhi alikutwa ameuwawa kikatiliki huki miguu yake ikiwa imefungwa kamba. Sr. Teifenbacher akikuwa nchini Afrika ya Kusini kwa takribani miaka 60. Amekuwa akitoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Huyu ni mtawa wa pili wa Shirika la Masista wa Damu Takatifu ya Yesu kuuwawa katika kipindi cha muda mfupi nchini Afrika ya Kusini.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican. 








All the contents on this site are copyrighted ©.