2015-04-20 10:02:00

Siku ya Kuombea Miito Duniani: Mashemasi 19 kupewa Daraja la Upadre


Katika maadhimisho ya Jumapili ya Nne ya Kipindi cha Pasaka, tarehe 26 Aprili 2015 maarufu kama Jumapili ya Kristo Mchungaji mwema, ambayo ni siku maalum kwa ajili ya kuombea Miito Mitakatifu ndani ya Kanisa, Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kuongoza Ibada ya Misa Takatifu kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican pamoja na kutoa Daraja Takatifu la Upadre kwa Mashemasi 19 kutoka Jimbo kuu la Roma.

Ibada ya Misa Takatifu inatarajiwa kuanza saa 3: 30 kwa saa za Ulaya. Itakumbukwa kwamba, Mashemasi watakaopewa Daraja Takatifu la Upadre, kumi na watatu ni wale wanaotoka katika Seminari kuu za Jimbo kuu la Roma; Mashemasi tisa wamepata majiundo yao ya kikasisi kutoka katika Seminari ya “Redemptoris” na Mashemasi watatu wanatoka katika Seminari kuu ya Kipapa la Jimbo kuu la Roma na Shemasi mmoja, ameandaliwa kutoka katika Seminari ya “Madonna del Divino Amore”.

Kardinali Agostino Vallini kwa muda wa juma zime anatoa mafungo kwa Mashemasi hawa kama sehemu ya maandalizi ya kujongea kwenye Daraja Takatifu la Upadre. Ijumaa, Jioni tarehe 24 Aprili 2014 kutakuwa na mkesha wa Sala kwa ajili ya kuombea miito kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Yohane wa Laterano.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.