2015-04-17 09:02:00

Papa Francisko kutembelea nchi za Amerika ya Kusini: 6-12 Julai, 2015


Baba Mtakatifu Francisko amekubali mialiko iliyotolewa na Maaskofu pamoja na wakuu wa nchi kutoka katika nchi kadhaa za Amerika ya Kusini na kwamba, ameamua kuzitembelea nchi hizi kuanzia tarehe 6 hadi 12 Julai 2015. Padre Federico Lombardi msemaji mkuu wa Vatican anabainisha kwamba, Baba Mtakatifu anatarajiwa kufanya hija ya kitume nchini: Ecuador kuanzia tarehe 6 hadi tarehe 8 Julai 2015.

Papa atakuwa nchini Bolivia kuanzia tarehe 8 hadi tarehe 10 Julai 2015. Baba Mtakatifu atahitimisha hija yake ya kitume Amerika ya Kusini kwa kutembelea Paraguay kuanzia tarehe 10 hadi tarehe 12 Julai. Padre Federico Lombardi anasema kwamba, ratiba rasmi kwa ajili ya hija hii ya kitume inatarajiwa kutolewa wakati wowote kuanzia sasa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.