2015-04-16 10:08:00

Baraza la Ushauri la Papa lakamilisha kikao chake


Washauri wa karibu wa Papa Francisco ambao ni Makardinali tisa, Jumatano, walikamilisha  kikao chao hapa Vatican. Katika kikao hiki wamejadili masuala mbalimbali yanaohusiana na maoni yanayotafuta kufanya mabadiliko katika Idara za Vatican ambazo hujumuishwa kama ofisi za “ Curia ya Roma”. Na hasa walilenga katika mapendekezo yanayotaka kuunda upya mfumo wa vyombo vya habari Vatican, na pia suala la wajibu wa Askofu katika kuwashughulikia watumishi wa Kanisa wanaotuhumiwa kuhusika na madhulumu ya ngono kwa watoto .  

Mkurugenzi wa Habari Vatican, Padre Federico Lombardi , Jumatano mapema alitoa muhtasari kwa wanahabari juu ya kikao hicho, kwamba, kikao hiki cha Makardinali tisa ,  cha siku tatu,  kilichoanza Jumatatu 13-15  2015, ndani ya Vatican, kilifanyika katika hali ya faragha .  Na kimejadili zaidi , juu ya kazi za kufanya mageuzi katika ofisi za Curia ya Roma katika mambo mawili: kwanza ni  mbinu zinazoweza tumika kwa ajili ya utendaji wa kazi  kwa mwaka 2015 na 2016 ili kusonga mbele  na  ufanisi wa kazi ya kuandaa Katiba mpya, na tafasiri ya  hatua zinazolengwa kuchukuliwa na Makardinali  kwa ajili ya kufanya mageuzi katika Idara za  Curia, kama ilivyopendekezwa  wakati  mkutano wa Makardinali wa kawaida, “Consistori “  hivi karibuni (ambamo  mna hotuba zaidi ya 60 juu ya somo hili na vidokezo muhimu kwa mwanga  Dibaji ya Katiba, na vipengele maalumu kwa ajili ya mageuzi).  Padre Lombardi  ametaja  mwelekeo zaidi ni katika uundaji wa idara  mbili zitakazokuwa na uwezo zaidi,  moja ikiwa kwa ajili ya huduma ya misaada,  haki, amani, na nyingine kwa ajili ya  walei, familia, maisha.  

Jambo jingine lililozungumzwa na  Baraza ni juu ya uundaji upya mfumo wa vyombo vya habari vya Vatican, kama ilivyopendekezwa na  kamati maalum inayoongozwa na Bwana Chris Patten ambayo iliwasilisha ripoti yake ya mwisho. Papa Francisco hivi karibuni anatazamiwa kutaja mabadiliko mapya kama itakavyokuwa imeundwa katika mpango wa utekelezaji kwa ajili ya kupunguza gharama za uendeshaji nauratibu kwa vyombo vya habari Vatican.

Hatimaye, Padre Lombardi , alieleza kwamba , Baraza limezungumzia wajibu wa Kanisa kwa  tuhuma zinazotolewa dhidi ya Mapadre au Maaskofu au watawa au Wakuu wa mashirika katika kesi hasa zinazohusiana na madhulumu ya ngono kwa watoto. Hoja iliyowasilishwa na  Kardinali Sean  O'Malley, Rais wa Tume mpya kwa ajili ya ulinzi wa watoto. Tume yake ilipenda kushirikishana mawazo na Papa hasa wakijali kilichotokea kwa Askofu wa Chile , anayetuhumiwa kwamba amekuwa akifunika funika kesi za Mapadre waliotuhumiwa kuhusika na madhulumu ya ngono kwa watoto, licha ya Kanisa kutoa mwongozo wazi jinsi ya kuwashughulikia  wahalifu hao. Kardinali O’Malley aliweka wazi kwamba , hili ni jambo linalotakiwa kutolewa maamuzi haraka hasa katika kusimamisha mara moja  , mamlaka ya wale wanaoshindwa kusitisha uhalifu huu katika maeneo.   Tume,  imependekeza Papa na Baraza lake kulishughulikia suala la "Uwajibikaji" na  "Wajibu" kuhusiana na ulinzi wa watoto, kwa  kutaja utaratibu na mipango sahihi yatathmini na kuhukumu katika kesi za  "matumizi mabaya ya ofisi" katika uwanja huu, hasa na watu wenye wajibu katika Kanisa.
 








All the contents on this site are copyrighted ©.