2015-04-15 15:14:00

Katekesi ya Papa juu ya familia : yalenga katika usawa kati mme na mke


Baba Mtakatifu katika Katekesi yake kwa mahujaji na wageni, ameonyesha kujali kwamba, bado juhudi zaidi zinahitajika, kwa ajili ya kufanikisha usawa na uelewa kamili juu ya tofauti za kijinsia kati ya mwanamke na mwanamme katika maisha ya  kijamii na kikanisa pia . Sauti ya wanawake ni lazima isikilizwe na maoni yake kupewa uzito hasa wakati wa maamuzi. Papa alitoa msisitozo huo , mapema Jumatano hii, akiendelea na katekesi yake juu ya mada ya familia, sehemu ya kumi,  ambamo ameangalia zaidi kiini cha familia ambacho ni Mme na Mke. Amesema ni zawadi kubwa ya Mungu kwa wanadamu, kwa kumuumba  kwa mwanamume na mwanamke na kuwaunganisha pamoja katika sakramenti ya ndoa.  Papa alitazama kwa makini zaidi juu ya tofauti za kimaumbile kati ya mwanamume na mwanamke, katika kilele  cha uumbaji wa Mtakatifu  wa Mungu.

Mafundisho ya Papa, yamenukuu zaidi Maandiko Matakatifu ya Biblia juu ya  uumbaji , kama ilivyoandikwa katika  kitabu cha Mwanzo, akisema,  tunasoma kwamba Mungu, baada ya kuumba ulimwengu na viumbe vyote, aliikamilisha kazi yake ya uumbaji kwa kumuumba binadamu kwa mfano wake mwenyewe: "kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba" (Mwanzo 1: , 27),ndivyo kinavyosema kitabu cha Mwanzo.

Papa aliendelea kuzungumzia tofauti za kijinsia zilizoko katika mfumo wa Maisha, lakini akisisitiza kwamba , wote wawili, mwanamume na mwanamke, hubeba ndani yao  sura na mfano wa Mungu, kama maandiko Matakatifu ya Biblia yalivyorudia kutaja  mara tatu katika mistari miwili (26-27). Mwanamume na mwanamke ni sura na mfano wa Mungu.  Hii inatuambia kwamba si tu mwanaume aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu, na wala si tu mwanamke aliyeumbwa kwa sura na  mfano wa Mungu, lakini ni wote wawili  mwanamume na mwanamke, kama wanandoa, wao ni mfano wa Mungu. Na tofauti ya maumbile kati ya mwanaume na  mwanamke si kwa ajili ya upinzani, au mmoja kuwa chini ya mwingine ,  lakini kwa ajili ya  ushirika na mwendelezo wa kizazi, daima wote wawili wanaendelea kuwa katika sura na mfano wa Mungu.

Papa anasema, uzoefu unatufundisha  kujua  vizuri zaidi na kukua katika  ushirikiano wa binadamu kwa ajili ya kukamilishana katika  mahitaji ya maisha yenye  usawa kati ya mwanaume na mwanamke. Kumbe hakuna madhara kati ya tofauti hizi za kimwili. Wote wawili wameumbwa kwa ajili ya kusikilizana na kusaidiana. Papa ameeleza na kuasa kwamba,  bila kuwa na  utajiri  wa kuheshimiana , iwe katika mawazo , au katika mahusiano,  upendo na kazi, pia katika imani , wote wawili hawawezi kuelewa kwa kina  nini maana ya kuwa mwanaume na mwanamke.

Papa aliendelea kutazamisha katika utamaduni wa kisasa, ambao umefungua nafasi mpya , uhuru mpya na kina kipya  kwa ajili ya utajiri wa ufahamu  katika utofauti huu.  Lakini pia umezua pia mashaka mengi na ubabe mwingi.  Papa  kwa mshangao alitoa mfano wa nadharia zinazotafuta  uwepo wa tofauti hizi katika haja za kujamiiana katika ngono eti tu kwa  sababu wao hawawezi tena kukabiliana nayo.  Amelitaja hili ni tatizo kubwa linalohitaji kujadiliwa zaidi, ili kujua zaidi kwa kina juu ya upendo  wa kweli kati ya mwanaume na mwanamke katika maisha ya ndoa.  Iwapo kuna kasoro ni lazima kutibu kwa heshima na kushirikiana na urafiki. Papa anasema  pamoja na mapungufu haya ya kibinadamu, kwa mkono na neema ya Mungu, inawezekana kuwa na  muungano ndoa na familia kwa ajili ya maisha. Dhamana ya ndoa na familia ni jambo zito na muhimu  kwa kila mtu, si tu kwa Waumini.  Papa alihimiza wasomi kutoiweka pembeni mada hii, kama vile ni si jambo la msingi katika utendaji wa jamii iliyo huru zaidi na haki zaidi.

Papa alikamilisha mafundisho yake kwa kutazama wajibu wa Kanisa katika hili akisema, huu ni wajibu mkubwa wa Kanisa, waamini wote, na  hasa familia za waamini, zinapaswa  daima kugundua  upya,  uzuri wa ubunifu wa Muumbaji  katika kuwaumbe mke na mme kwa mfano wa Mungu.  Na  ndivyo mwanamume na mwanamke  hutafutana kati yao  pamoja na  Mungu. 

Papa ametaja changamoto iliyoko mbele ya Kanisa na waamini na familia leo hii hasa ni katika kungundua uzuri wa mpango wa Mungu, katika utumilifu wa kazi yake ya kuumbua mtu kwa sura na mfano wake. . 








All the contents on this site are copyrighted ©.